Mkutano waandaliwa kujadili uharibifu wa mkaa Somalia

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/mkutano-waandaliwa-kujadili-uharibifu.html

Mkutano wa siku mbili umeanza mjini Mogadishu nchini Somalia, wenye nia ya kujadili uharibifu wa mazingira unaosababishwa na uzalishaji wa mkaa.
Umoja wa Mataifa unasema kila baada ya sekunde 30 mti mmoja hukatwa kutengeneza mkaa nchini Somalia, hali inayosababisha madhara makubwa kama vile ukame na mafuriko, pia ufadhili wa mzozo nchini humo.
Umoja wa mataifa unakadiria kuwa usafirishaji wa mkaa una gharama ya zaidi ya pauni milioni 74 kwa mwaka na sehemu ya faida huenda kwenye makundi ya wanamgambo, al-shabab
walinda amani wa Kenya wameshutumiwa kuwezesha vitendo vya usafirishaji haramu wa mkaa kupitia bandari ya Kismayu
Mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, Michael Keating amesema ongezeko la watu, mabadiliko ya hali ya hewa, na uharibifu wa mazingira vinachangia ''matatizo mengi'' yanayowakabili wasomali wanaopigania mali asili kama vile ardhi, mbao na maji, hali ambayo inachochea mizozo.
Takriban watu milioni 2.2 wameyakimbia makazi yao ndani ya Somalia na wengine 870,000 wamesajiliwa kama wakimbizi katika nchi nyingine.Umoja wa mataifa umeeleza
Baadhi ya watu wamekimbia mapigano, wengine wamelazimika kukimbia mashamba yao kutokana na ukame.
Keating amesema kuwa pamoja na maeneo mengi kukosa umeme, bado Somalia ina nafasi ya yakupata huduma hiyo kwa kutumia gridi ya nchini humo kwa kutumia nishati mbadala.
Uhitaji ni mkubwa, huku ripoti ya maendeleo ikionyesha kuwa asilimia 30 pekee ya raia wa Somalia walikuwa na umeme mwaka 2016 kutoka asilimia 20 mwaka 2010.
Asilimia 2 pekee wanatumia mafuta masafi kwa ajili ya kupikia, huku wengine wakitumia mafuta machafu kama mafuta ya taa na mkaa ambavyo vinaathiri afya zao
Mjumbe huyo amekuwa na mazungumzo na serikali kuona kama Somalia inaweza kuwa nchi inayotumia nishati safi na salama kama vile solar, nishati itokanayo na upepo na maji kutoka kwenye mito yake miwili mikubwa.