Kumbukizi ya mwaka mmoja ya ajali ya watoto wa Lucky Vincent yaibua kilio upya Arusha.

Wazazi, walimu na wanafunzi wa St Lucky Vincent
Image captionWazazi, walimu na wanafunzi wa St Lucky Vincent
Simanzi na majonzi kutoka kwa wazazi, walimu na wanafunzi wa St Lucky Vincent zilirejea upya katika kumbukumbu ya ajali iliyouwa watoto 32, walimu wawili na dereva mmoja mnamo Mei 6 2017.
Mamia ya watu walihudhuria kumbu kumbu hiyo iliyoanza kwa ibada na baadae hotuba mbalimbali pamoja na kuweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu uliojengwa katika shule hiyo.
Hata hivyo macho ya wengi yalikuwa kwa manusura watatu ambao walitaja kuwa ni watoto wa miujiza.
Manusura hao ambao ni Doreen Elibariki, Wilson Tarimo na Sadia Awadh, kila mmoja kwa nafasi yake waliweza kutoa shukrani zao za dhati kwa huduma ya afya huko nchini Marekani na kupata ufadhili wa elimu nzuri ya sekondari.
Wageni waliweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu uliojengwa katika shule hiyo
Image captionWageni waliweka mashada ya maua katika mnara wa kumbukumbu uliojengwa katika shule hiyo
Sadia mwenye umri wa miaka kumi na nne, anasema alipoteza kumbukumbu kwa muda baada ya ajali na kukiri kuwa alijikuta yuko nchi ya kigeni mara baada ya tukio hilo.
Aliongeza kuwa ana kila sababu ya kushukuru kwa kupata nafasi nyingine katika maisha.
''Sasa anaweza kukumbuka jinsi dereva alivyoshindwa kulihimili gari mpaka ajali ikatokea" alisimulia.
Polisi watumia nyimbo kukabili ajali za pikipiki Tanzania
Kwa upande wa wazazi, Msaghaa Kimia ambaye naye alipoteza mtoto wake alisema huu ni wakati sasa wa kuondoa chuki zote, lawama, kwa wale waliokwaruzana au kukosana wanapaswa kusamehehana.
" Hakuna jambo lingine la muhimu katika siku ya leo zaidi ya kusameheana'' Kimia alisisitiza.
Manusura wa ajali kutoka shule ya Lucky Vincent
Image captionManusura wa ajali kutoka shule ya Lucky Vincent
Aliongeza kwa kudai ajali inaweza kutokea popote, hivyo watu hawapaswi kuangalia kwenye usafiri tu bali hata kwenye majengo ya shule.
Mkuu wa shule hilo anasema pamoja na pigo kubwa lililowakuta, anashukuru kuwa wazazi walikuwa pamoja naye na kumpa moyo.
Aliishukuru serikali kwa kutoa wataalamu wa kisaikolojia ili kuweza kuwarejesha watoto kwenye hali yao ya kawaida maana anasema athari iliwapata wote hata wale waliokuwa hawajapata ajali.
Aidha wamiliki wa shule nyingine wamesema wazazi kwa kipindi hiki wamekuwa wagumu kulipia safari za masomo haswa wakati huu wa mvua kutokana na uoga waliopata baada ya ajali ya basi la shule ya Lucky Vincent.

Related

habari 8835430196796853763

Post a Comment

emo-but-icon

item