Kanisa la Kianglikana kuuza makanisa 133

http://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/kanisa-la-kianglikana-kuuza-makanisa-133.html

Kanisa la Kianglikana huko Tasmania lina mpango wa kuuza nusu kati ya makanisa yake 133 ili kusaidia kuwalipia wahasiriwa wa kijinsia walionyanyaswa walipokuwa watoto.
Waumini katika jimbo hilo lililopo kusini mwa Australia wamekasirishwa na hatua hiyo ya kuyapoteza makanisa hayo ambayo yana zaidi ya miaka 130 , lakini manusura wamesema hatua hiyo ni ujumbe muhimu wa kupata msahama kutoka kwa Mungu.
Uuzaji huo unatarajia kupata US$6 kuwasaidia wahasiriwa hao.
Kasisi mkuu wa Tasmania , Richard Condie amesema ' uchungu' wa kuyauza makumi ya makanisa hayo ni hatua ambayo itawapatia manusura wote wa unyanyasaji wa kingono haki.
Malipo ya wahasiriwa ni swala muhimu kwa kamati ya Royal iliyobuniwa miaka mitano iliopita kuchunguza walionajisiwa walipokuwa watoto katika vyuo nchini Australia.

Waumini wengine huko Tasmania wamesema wameshangazwa na kutamaushwa kwa uuzaji huo, huku wanaounga mkono wamekaribisha uamuzi wa kanisa hilo la Kianglikana.
Zaidi ya malalamishi ya 1,100 ya visa vya unyanyasaji wa kingono vimeripotiwa dhidi ya kanisa hilo la Australia, kamati hiyo ya Royal imesikiliza kesi hizo.
Madai hayo yameorodheshwa kutoka mwaka 1980 hadi 2005 , yametajwa dhidi ya makanisa 569, yakiwajumuisha wahubiri 247.
Kanisa la Kianglikana limekiri kukubali kuwanyamazisha wahasiriwa hao ili kuhifadhi hadhi yao.
Kasisi mkuu wa Melbourne, Philip Freier amesema ''aliaaibika sana'' kwa majibu wa kanisa hilo.
Mwezi wa Februari , zaidi ya watu 4,400 wanadaiwa kunyanyaswa na kanisa katholiki la Australia wakati kama huo miaka 35 iliyopita.