Tusipimane ubavu : RC Makonda

MKUU  wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda,  amewatahadharisha wanaume  wanaodhani wanaweza kukaidi wito  wa kufika ofisini kwake baada ya kulalamikiwa kutelekeza watoto  ambapo amewatumia salamu kwa kuwaambia  wasimjaribu wala kupima mamlaka aliyonayo.
RC Makonda  ametoa kauli hiyo wakati wa mahojiano  ya kipindi cha tathimini ya Zoezi la kudai haki za watoto waliotelekezwa* ambapo amesema tangu jumatatu zaidi ya 17,000  walifika ofisini kwake na Kati ya hao 4,400 wamesikilizwa.

Aidha RC Makonda  amesema kinachomfariji  ni kuona idadi kubwa ya kinababa wanaofika ofisini kwake wanakubali kumlea mtoto* ambapo hadi sasa  familia 295  zimekubali kuhudumia mtoto na familia 29  zimepima DNA

Hata hivyo RC Makonda  amesema baada ya zoezi hilo ataunda tume ya kuangalia changamoto zilizopo katika sheria ya matunzo ya mtoto* kisha kuifikisha kwa waziri  husika kwaajili ya kufikishwa Bungeni  kwaajili kufanyiwa marekebisho.*

Pamoja na hayo *RC Makonda  amesema hatoyumbishwa na baadhi ya  watu wasiojua uchungu wanaopata kinamama  kwa *kubeza  zoezi hilo kwakuwa yeye ametambua *Mateso waliyokuwa wakipata kinamama* waliotelekezwa.

RC Makonda  amesema ikitokea mwanamke aliefika ofisini kwake na kumshitaki mwanaume aliezaanae kisha uchunguzi ukafanyika na kubaini  udanganyifu mwanaume anayo  haki ya kufungua kesi ya kudhalilishwa na afisa ustawi wa jamii wa mkoa atalazimika kuwa shahidi mahakamani.

":WATU WENYE DHAMBI WANAPENDA GIZA NDIO MAANA UKIWASHA NURU WANAIBUKA KUPINGA".RC MAKONDA 

Related

habari 6719008682104659613

Post a Comment

emo-but-icon

item