IYF yaingia mkataba na Chuo kikuu huria cha Tanzania




SHIRIKA lisilo la kiserkali linalojishughulisha kusaidia Vijana wa Kitanzania kutoka Korea Kusini, IYF leo limeingia makubaliano ya kimkataba na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Jijini Dar es Salaam.
Makubaliano hayo yamesainiwa ikiwa na lengo la kushirikiana kwa dhati katika kutoa mafunzo kwa wanafunzi wanaosoma chuo hicho na IYF .
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya IYF, kutoka Makao makuu ya Kurea Kusini, Seon Kim, amesema lengo la mkataba ni baada ya kuona  fursa iliyopo chuoni hapo na kuamini Vijana wengi watafikiwa na elimu ya moyo katika kuwafundisha uwajibikaji na kujitegemea ili kuleta maendeleo kwa Taifa.
Amesema Tanzania ni miongoni mwa Mataifa yanayokabiliwa na  changamoto mbali mbali ikiwemo ajira na utawala bora, hivyo  kuwa karibu na Vyuo vikuu hapa nchini kutasaidia kuwajengea Vijana wa Kitanzania uwezo mkubwa wa kufikiri na kuwa na mitizamo  chanya ya kimaendeleo badala ya kubweteka mitaani wakidai ajira hakuna.


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof. Elifasi Bisanda  kulia akisaini mkataba na shirika la Korea la IYF lenye lengo la kuwajengea uwezo vijana kuhusu elimu ya moyo/kujitegemea, na kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa IYF Bw. Song Hun Kim akisaini mkataba wa makubaliano wa shirika hilo na Tanzania.
“Elimu ya moyo inahitajika sana kwa sasa kutokana na  ujio wa utandawazi Vijana wengi wanapotea na wengi wao hutumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii kwa kuangalia masuala ya kipuuzi na kujikuta wakiingia katika wimbi la maovu”amesema Kim.
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu Huria cha Dar es salaam Prof. Elifas Bisanda akibadilishana mikataba na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la IYF Bw. Seong Hun Kim mapema jana katika Chuo Kikuu Huria jijini Dar es salaam.
Naye Mkamu Mkuu wa Chuo Huria cha Tanzania, Prof: Elifas Bisanda, ameushukuru Uongozi wa IYF kwa kuwapa fursa ya kushiriki kikamilifu katika jitihada za kumkomboa Kijana wa Kitanzania.


Bandi ya IYF ikitoa burudani mbele ya meza kuu mapema jana Chuo Kikuu Huria jijini Dar es alaam
Bisanda, amesema ushirikiano uliopo utaleta tija kwa Vijana wa Tanzania na kuwasaidia kupunguza wimbi la uharifu na utumiaji wa dawa za kulevya.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Prof. Elifas Basinda akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kusaini mkataba na Shirika la YIF mapema jana jijini Dar es salaam.
Aidha, amesema katika maendeleo  kuna vitu vipya vinaingia na kubaidlisha maisha ya watu katika mitazamo hasi, hivyo ujio wa IYF hapa nchini utapelekea kubadili fikra za Vijana katika kuondokan na dhana ya kuajiriwa badala yake watatafuta maarifa mapya ya kujiajiri kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea ikiwamo Korea Kusini.

Viongozi wa Shirika la IYF wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Dar es salaam baada ya kumaliza tafrija fupi ya kusaini mkataba wa makubaliano wa chuo hicho na shirika la nchini Korea la IYF.
“Watu wanofanya biashara za Magendo wamekosa elimu ya moyo, hivyo wanajikuta wanaitia Taifa hasara kwa kutolipa kodi”,amesema Bisanda
Afisa Habari IYF , Mwanzani Ramadhani 
Amesema moja ya mambo waliyokubaliana katika mkataba huo ni pamoja na kuwawezesha waalimu kwa ajili ya kubadilsiah fikra za wanafunzi.


Katika makubaliano hayo ya mkataba,  kumekuwa na zoezi la kuwafundisha Waalimu mbali mbali wa Shule za Sekondari Mkoa wa Dar es Salaam ambapo jumla ya Waalimu 400 walihudhuria mafunzo hayo.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

habari 7756324297607097299

Post a Comment

emo-but-icon

item