Watoto ,Vijana wafundishwa kuwa na utaratibu wa kuweka akiba fedha Benki.
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/watoto-vijana-wafundishwa-kuwa-na.html
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB Tanzania, Ineke Bussemaker(wa kwanza kulia) akizungumza katika hafla hiyo |
WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,nchini Ummy Mwalimu, amewataka wazazi kuweka utaratibu wa kuwawekea watoto wao akiba ya fedha katika akaunti ya Wajibu ya benki ya NMB, kwa ajili ya matumizi ya baadaye.
Ummy aliyasema hayo wakati akizindua kampeni ya uhamasishaji wa elimu ya utunzaji wa fedha inayojulikana kama Jifunze, Jipange, Wajibika iliyoanzishwa na benki hiyo.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akizungumza kwenye uzinduzi huo |
“Nimefurahi NMB mmeamua kwenda kufunza watoto WAJIBIKA, tatizo Watanzania kwenye matumizi yetu hayana kipaumbele kama mfano kutuza fedha watu katika burudani mbalimbali ambapo watu hutoa pesa nyingi lakini hawana utaratibu wa kuwawekea watoto akiba katika mabenki.
Baadhi ya wanafunzi walioshiriki wakiwa kwenye
picha ya pamoja na mgeni rasmi
|
Pia , Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker, alisema NMB inatambua umuhimu kwa watoto kujua ulazima wa kujiwekea akiba, hivyo ilianzisha kampeni hiyo ili kuwasaidia watoto kupata elimu ambayo wanaamini kwamba wakielimishwa , itawasaidia kwa miaka ijayo kuwa na kizazi ambacho kitakuwa kinaweka akiba ya baadaye.