Vikombe 3 vya kahawa kwa siku 'vinaweza kuwa na faida za kiafya'

Unywaji wa kahawa kiasi ni salama , na vikombe vitatu kwa siku vya kahawa vinaweza kuwa na faida kadhaa za kiafya , kulinga na utafiti uliofanywa na BMJ.
Utafiti huo ulibaini kuwa unywaji wa kiasi hicho cha kahawa unaweza kumfanya mnywaji kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya ini na saratani na kupunguza kiwango cha klupata kiharus - lakini watafiti hao wanasema hawawezi kuthibitisha kuwa kahawa ndio sababu ya upungufu wa athari hizo .

Unywaji wa kiwango kikubwa cha kahawa wakati wa ujauzito uhaweza kuwa hata hatari , umethibitisha utafiti huo.
Wataalam wanasema hata hivyo kuwa watu hawapaswi kuanza kunywa kahawa kwa sababu za kiafya ama kama njia ya kuzuwia magonjwa.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Southampton walikusanya taarifa kuhusu athari za unywaji wa kahawa kwa binadamu kwa mwili wa binadamu kwa ujumla , wakizingatia tafiti zaidi ya 200 , ambazo nyingi kati yake zilikuwa za uchunguza.
Watafiti walipolinganisha watu wasio kunywa kahawa , na wale wanaokunywa takriban vikombe vitatu vya kahawa kwa siku walionekana kupunguza uwezekano wa kupata kiharusi.
Faida kubwa ya unywaji wa kahawa zilionekana katika kupunguza hatari ya ugonjwa wa ini, pamoja na saratani.
Lakini Profesa Paul Roderick, mmoja wa waandishi wa utafiti huo kutoka kitivo cha tiba katika Chuo Kikuu cha Southampton, anasema utafiti huo haukusema ikiwa unywaji wa kiasi fulani wa kawaha ulileta ulikuwa na mabadiliko fulani.
"Masuala kama vile umri,ikiwa watu walikuwa ni wavutaji wa sigara au hapana na ikiwa walifanya mazoezi ya kimwili kwa kiasi fulani pia yalichangia katika athari za unywaji kahawa ," alisema.
vikombe vya kahawaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKila kitu kwa kiasi, ukiwemo unywaji wa kahawa
Utafiti huu unaunga mkono tafiti na uchunguzi wa hivi karibuni wa unywaji wa kahawa wa kiwango hicho
Watafiti wanasema kuwa wanywaji wa kahawa wanapaswa kunywa kinywaji hicho "kwa kuzingatia afya " - ikiwa ni pamoja na kuepuka matumizi ya sukari nyingi, maziwa au kunywa na vitafunio vyenye mafuta.
Na wanatoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu ya juu ya unywaji wa kahawa ili kubaini zaidi faida za kiafya zinazoweza kutokana na unywaji wa kahawa.
Watu wakinywa kahawa na kitafunio vya aina ya croissantsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNi vema unapokunywa kahawa kuepuka kula vitafunio vyenye sukari
Kwa sasa wachunguzi wanakabiliwa na kibaruia cha kubaini ni kiwango kani hasa cha kahawa kinachoweza kuwa na faida ya kiafya jambo ambalo bado ni gumu.

Related

MAKALA 2546038327123588891

Post a Comment

emo-but-icon

item