Mnyate aikacha Simba
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/12/mnyate-aikacha-simba.html
Mshambuliaji asiye namba kwenye kikosi cha Simba Jamal Mnyate, ameandika barua kwa uongozi wa timu hiyo aruhusiwe aondoke.
Awali, kulikuwepo na taarifa za mshambuliaji huyo kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.
Mchezaji mwingine anayetajwa kuachwa ni mshambuliaji Juma Liuzio ambaye yeye uongozi wa Simba umepanga kumtoa kwa mkopo.
Mnyate ameomba aachwe ili akajiunge na Lipuli FC inayonolewa na Selemani Matola.
Tayari Mnyate amekutana na mabosi wake huku akiahidiwa kupatiwa barua hiyo ya kuondoka Simba baada ya kukosa nafasi ya kucheza.