Meya wa jiji la Dar Mwita ahudhuria mkutano wa kujadili utawala bora Nchini Marekani

MSTAHIKI Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita leo ameondoka jijini hapa kuelekea Chicago Nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa Mameya kutoka sehemu mbalimbali duniani utakaofanyika Desemba 4 hadi 7 mwaka huu.


 Mkutano huo unatarajiwa kuhusisha Mameya 182 kutoka sehemu mbalimbali Dunia ambapo pamoja na mambo mengine watajadili suala la utawala bora pamoja na utumishi wa viongozi kwa wananchi.

Aidha katika mkutano huo pia wataangalia na kujadili changamoto za majiji makubwa hususani katika sekta ya Afya, miundombinu, Maji safi na salama, Elimu pamoja na mabadiliko ya tabia ya Nchi.

Image result for meya mwita marekani

Desemba  5 Mameya wote waliohudhuria mkutano huo kwa pamoja watashindanisha majiji yaliyofanya vizuri katika sekta ya miundombinu ambapo jiji la Dar es Salaam limeingia kwenye ushindani huo kupitia  mradi wa mabasi yaendayo haraka.

Aidha katika ushindani huo, Meya Mwita amesema kuwa ana amini kwamba jiji la Dar es Salaam litaibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa kuwa mradi huo umekuwa ukifanya vizuri katika sekta ya  usafirishaji na kwamba watanzania wajiandae kwa ajili ya kupokea tuzo hiyo.

Majiji mengine ambayo yanameingia kwenye ushindani huo mbali na jiji la Dar es Salaam ni Mji wa Cape Town, Cairo pamoja na majiji mengine Dunia. Meya Mwita atarajea Nchini Desemba 8 mwaka huu.

Related

habari 3931518150329762875

Post a Comment

emo-but-icon

item