RC Makonda aahidi ushirikiano kwa Mabaharia
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/rc-makonda-aahidi-ushirikiano-kwa.html
MKUU wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameahaidi kutoa ushirikino kwa mabaharia wote nchini ili
kuweza kutatua changamoto zao ikiwemo kifedha, ajira pia katika kukamata mizigo
ya magendo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh Paul Makonda akihutubia semina elekezi ya Mabaharia katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA SCOLASTICA MUNDE )
|
Alisema hayo katika semena elekezi ya mabaharia iliyo
fanyika hivi karibuni katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es salaam ili kuwajengea uwezo mabaharia na kutambua sheria zilizowekwa.
Mabaharia wa Meli jijini Dar es salaam wakishusha mfano wa Meli kwa ajili ya kumkabidhi Mkoa wa Dar es Salaam. Paul makonda . ( PICHA NA MOHAMED ALLY)
|
“Kikubwa muwe na ushirikiano mkubwa, nazijua changamoto zenu na ninauwezo
wa kuzitatua pia munajukumu kubwa la kutunza rasilimali ya nchi yetu, kwani tukishirikiana
pamoja tunauwezo wa kukamata mizigo ya magendo
inayoingizwa nchini na wakwepa kodi”Alisema.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mabaharia nchini , Kapteni Josayah Mwakibuta akiepeana mkono na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, RC Makonda mara baada ya kukabidhi mfano wa Meli hiyo. (PICHA NA MOHAMED ALLY)
|
Kadhaarika Makonda amewataka mabaharia
kufuata sheria za kazi hiyo ikiwa
pamoja na kudhingatia usalama wa Raia
pindi wawapo kwenye vyombo vyao ili kuepuka migogoro na Ajari.
“Mabaharia nyinyi ni wachapakazi na Majasili kila siku mnabeba dhamana kubwa ya watu na
mali zao hivyo nimuhimu kuzingatia sheria za vyombo vyenu ili kuepukana migogoro na wakaguzi wa vyombohivyo,
niwa ahidi kuwapigania katika kuhakisha
mabaharia munapata ajira ndani na nje ya nchi kwasasa tuna wabobezi wa vyombo
hivyo sio vyema kuona mgeni anafanyakazi huku mwenyeji hana kazi”Alisema
Kwa upande wake katibu mkuu wa chamahicho nchini Seafarers Union (Tasu) , Kapteni Josayah
Mwakibuta alisema lengo la kufanya semina hiyo elekezi ni kuwataka mabahaaria
kuelewa sheria na haki zao, tatizo la ajira na Mkataba wa muungano wa
sheria za kazi (MMC) uliokubaliwa na
bunge wenye lengo la kuungana katika kutoa ajira nje ya nchi.
"Tunataka waelewe lengo la semina hii ili
kutambua lengo la kilichopokelewa na bunge juu ya mkataba wa (MMC), nikitu kizuri kitakachowezesha
kuongezeka kwa soko la Ajira kwa mahabaria kufanya kazi katika nchi za ulaya jambo ambalo lilikuwa
gumu kweo kupata
kazi nje ya nchi kupitia mkata huu watakubaliwa" alisema.
Wakati huohuo ameipongeza serikali kwa kudumisha hali ya usalama wa bahari jambo linalo fanya
kuongezeka kwa thamani ya bahari yetu.
“ Viwango vya bahari bado vipo juu hii nikutokana na
ripoti ya ukaguzi wa viwango vya bahari Duniani , Tanzania ni miongoni mwa nchi
zilizo kuwa kwenye (White list) na ambazo hazipo kwenye mfumo huo vyeti vyake
vitakuwa havitambuliki Duniani, kuna nchi nyingi zimeondolewa katika mfumo
huokutokana na viwango vyake vya baahari kushukaa hii nijuhudi inayo fanywa na
serikali”Alisema