DC Hapi awapongeza Walimu Kinondoni
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/dc-hapi-achagiza-awapongeza-walimu.html
MKUU wa wilaya ya kinondoni Ally Hapi amewapongeza walimu shule za msingi zilizopo katika manispaa hiyo baada ya kushika nafasi ya kwanza kitaifa, katika mtihani wa darasa la saba kwa mwaka huu.
Akizungumza leo wakati wa utoaji wa tuzo kwa shule ambazo zimeongoza, Hapi ametoa wito kwa walimu hao kuendeleza juhudi hizo pamoja na kushirikiana kwa pamja na kutoa mbinu zao zote ili kuhakikisha wanaendelea kushika nafasi hiyo.
Amesema ni jambo jema kuwapongeza na kuwatia moyo walimu sambamba na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya muunamo wa Tanzania Mh John Magufuli kwa kuleta sera ya Elimu bure ambapo utoro kwa wanafunzi umepungua kwa kiasi kikubwa na watoto wanahudhuria masomo kwa wakati hali ambayo pia imepelekea wazazi wengi kujitokeza kuandikisha watoto.
Nae Meya wa Manispaa Kinondoni Benjamin Sitta amewapongeza walimu wa shule za msingi za manispaa hiyo baada ya kutoa matokeo mazuri ya Darasa la saba yaliyo pelekea kuongoza kitaifa kwa mwaka huu.
Sitta amesema kufanya hivyo ni kutoa motisha na kuwapa moyo wadau wote walioweza kuanikisha ushindi huo.
Aidha amesema hatua hiyo itawafanya watanzania waelewe kwamba elimu bure ina matokeo makubwa katika maendeleo ya elimu.