Chishaku yataka Sanaa ya Kareti ipewe kipaumbele
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/11/chishaku-yataka-sanaa-ya-kareti-ipewe.html
CHUO cha mchezo wa kareti cha CHISHAKU kilichopo Gerezani Kariakoo Jijini Dar es Salaam, kimefungua rasmi shindano la 10 kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Ardhi Mlimani leo.
Akizungumza na Raia Tanzania Online, Mkurugenzi na mkufunzi wa Chuo hicho Master Jimmy, amesema mchezo huo haupewi kipaumbele kama ilivyo michezo mingine hivyo kukosa Timu ya Taifa yenye ushindani.
Master Jimmy, amesema kuwa, lengo la kuwa na mashindano hayo ni pamoja na kutaka kufahamu uelewa wa wanafunzi hao juu ya masomo yao.
Aidha, Master Jimmy, amesema kuwa shindano hilo sio mara yake ya kwanza kwani shindano hilo ni la kumi kufanyika na lilianza mwaka 2007.
Hata hivyo, Master Jimmy , amesema kuwa mbali na kuwashindanisha wana lengo la kuwajengea uwezo na ukakamavu pamoja na kujua mbinu za kujilinda katika kutenegeneza Vijana kuwa wazalendo wa Taifa lao.
“Tumeamua kuwa na mashindano haya kila mwaka lengo ni kujua mafunzo kama yameeleweka vizuri pamoja na kuwajengea uwezo binafsi wa kujilinda na kutengeneza furaha miongoni mwa Wazazi na watoto ili kuwafundisha jinsi ya kuishi pamoja na kujenge urafiki ulio na amani”. Amesema Master Jimmy
Naye Mgeni rasmi ambaye ni Mhariri Mkuu wa Habari Gazeti la Raia Tanzania kutoka TSN Media , Moris Lyimo, amesema ni zamu ya Serikali kupitia upya sheria ya JKT nakuwaingiza watoto hao katika mfumo rasmi utakao wapa fursa ya kuajiriwa na kujiajiri kuliko ilivyo sasa.
“Serikali inapaswa kuwaangalia watoto hawa, kama waliweza kuingiza uhamiaji kwenye sekta rasmi basi iwe na jukumu la kulinda vipaji hivi na sio kuvitumia kipindi cha matukio na kuwaacha kwani wakilelewa vizuri naamini tutapata Vijana safi wenye uzalendo wa kweli watao wakilisha Vyema Taifa letu kama michezo mingine “ Amesema Lyimo
Mbali na washindi wa medali , wapo walioibuka na ushindi wa jumla ambapo kundi C waliibuka kinara kwa kupata alama 1016, mshindi wa pili kundi G wakiambuilia alama 903 wakati mshindi wa tatu akitokea kundi E kwa alama 750
Chuo hicho kipo kwenye mpango wa kuandaa tuzo za washindi wa Belt mbali mbali kama Vile Yellow Belt, White Belt, Orange Belt, Green Belt, Blue Belt, shindano hilo linatarajia kufanyika February mwaka 2018.