CCM Wilaya ya Ilala yamuangusha Mbunge Waitara na Meya wa Ilala

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ilala kimemuangusha Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara katika chaguzi za Serikali za Mitaa kwa kushinda mitaa 11 katika Jimbo la Ukonga   ambapo Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) wamekuwa wasindikiza mitaa yote wamepigwa.
Akizungumza jijiji  Dar es Salaam mapema leo hii,  Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Ubaya Chuma, ameyasema  hayo wakati alipokuwa akiwapongeza Wenyeviti wake Wilayani humo pamoja na kamati zote zilizosimamia uchaguzi huo.

Chuma amesema katika chaguzi za Serikali ya Mtaa chama hicho kimeweza kufanya vizuri kwani pia kilio kingine CCM wameangusha Nyumbani kwa Meya wa Ilala (CHADEMA) Charles Kuyeko naye amepigwa chini baada mgombea wa CCM kuibuka kidedea Jimbo la Segerea Kata ya Bonyokwa.
" CCM Wilaya ya Ilala mwaka 2015 tulipigwa kwa sasa zamu yao hizi ni  dalili tosha tutafanya vizuri chaguzi zijazo 2019 na 2020 tutawachinja asubuhi, chama chochote cha siasa ni kama mpira, mechi imekwisha tumeshachukua ubingwa kinachofuata wajiandae katika chaguzi zijazo"amesema Chuma.


Aidha amesema uchaguzi ulikuwa wa huru na haki na kwa wale waliofanya fujo wote walikamatwa na kupelekwa katika vyombo vya sheria , na kilichobakia  baada kumalizika kwa uchaguzi huo ni kutoa elimu endelevu kwa kuwapa mafunzo makada wote   ili waweze kuzungumza lugha moja .

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wazazi Wilaya hiyo . Lucas Lutainurwa aliwapongeza wana CCM wote kwa kuonyesha mshikamano na kuibuka kidedea kwa ushindi mnono ambao umerudisha hadhi ya chama kwa kukosa ushindi muhula uliopita

Lucas amewataka Wenyeviti wapya 12 wa ccm ambao wameshinda katika mitaa hiyo Mara baada kuapishwa wafanye kazi kwa weledi wasibweteke. 

Pamoja na kuipongeza Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ilala  ambayo inaongozwa na Mkuu wa Wilaya Sophia Mjema kwa kuimarisha ulinzi 
"Naipongeza  kamati ya ulinzi na Usalama ya Wilaya imeweza kutenda haki  pamoja na jeshi lake la Polisi  kwa kazi nzuri, ila nataka niwaombe Wenyeviti wa Mitaa mshirikiane katika utekelezaji wa majukumu yenu sambamba na kutatua kero za wananchi ngazi ya mtaa kwa kutekeleza Ilani ya Chama "amesema Lucas.

Related

SIASA 3066206609585030619

Post a Comment

emo-but-icon

item