Ajibu awatahadharisha simba kuhusu Mkude

MSHAMBULIAJI  wa Yanga, Ibrahim Ajibu ameonekana kumpa moyo kiungo na nahodha wa zamani wa Simba, Jonas Mkude.
Ajibu amemuambia Mkude kuwa iko siku thamani yake itajulikana huku akimsifia kuwa kiungo bora kabisa.

Straika huyo wa Yanga amefanya hivyo kupitia akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

"Maestro midfield, ipo siku thamani yako itaonekana kaka," anaandika Ajibu.

Mkude amekuwa akiendelea kubaki benchi kwa muda wakati Kocha Joseph Omog amekuwa akimuamini zaidi James Kotei, raia wa Ghana.

Lakini katika mechi mbili zilizopita, inaonekana Omog ameanza kumuamini zaidi Mkude.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

michezo 2924134134605843879

Post a Comment

emo-but-icon

item