RC Makonda abadili gia vita dhidi ya Madawa ya Kulevya
http://raiatanzania.blogspot.com/2017/08/rc-makonda-abadili-gia-vita-dhidi-ya.html
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meshimiwa Paul Makonda leo amepokea ugeni wa Wanajeshi wa Jeshi la Maji kutoka Nchini China waliokuja Nchini kwa lengo la kuimarisha mahusiano ya kijeshi ambapo amesema atandeleea na mikakati ya kudhibiti uingizwaji wa Dawa za kulevya zinazoingizwa Nchini kwa kutumia Bahari ya Hindi.
Katika mazungumzo kati Mkuu wa Mkoa na kikosi cha Jeshi hilo amewasilisha ombi la kupatiwa Boti za kisasa zitakazotumiwa Jeshi la polisi katika kuimarisha Doria kwenye mwambao wa Bahari ya Hindi ili kukomesha Biashara za magendo ikiwemo ya Dawa za kulevya na Bandari bubu.
Ombi hilo la Boti limepokelewa kwa mikono miwili na Jeshi hilo ambalo pia limeonyesha kufurahishwa na namna Mheshimiwa Makonda anakali wananchi wake kwa kuhakikisha wako salama katika kazi zao za kila siku.
Aidha Jeshi hilo limemualika Mkuu wa Mkoa kwenda kutembelea Meli kubwa na ya kisasa ya Jeshi hilo ambayo tayari ipo nchini kwaajili ya kuona namna inavyofanya kazi.
Lengo la ujio wa Jeshi hilo Nchini kuimarisha mahusiano ya kijeshi baina ya Tanzania na China ili kwa pamoja waweze kupambana na uhalifu.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Majini la China Real Admiral Shen Hao amesema kuwa ombi la Mkuu wa Mkoa la kupatiwa Bodi za kisasa watalitimiza na kueleza kuwa wataendelea kuimarisha mahusiano ya kijeshi baina ya Tanzania na China.