Kumbilamoto atekeleza ahadi hii kwa Wanamichezo Vingunguti

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/10/kumbilamoto-atekeleza-ahadi-hii-kwa.html





NAIBU Meya Manispaa ya Ilala na Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto, Leo amekabidhi vifaa vya michezo kwa Mabondia Katika kata yake ikiwa ni ahadi aliyoitoa katika kampeni yake kipindi cha Uchaguzi.
Kumbilamoto ametoa gropsi hizo zenye ubora wa hali ya juu, huku akiwaahidi kuendelea kutoa ushirikiano.
Baada ya kutoa zawadi hiyo, amewataka wapendane na wajikite katika malengo ili kuweza kuipeperusha vyema Bendera ya Tanzania Kimataifa.
" Kubwa zaidi nawapongeza Wanamichezo Hawa kwani ni moja ya watu waliochangia kunipa ushindi wa kiti hiki cha Udiwani, nawaomba wawe na mshikamano ili kufikia malengo kama ilivyo kwa wakina Matumla, Cheka na Wanamasumbwi wengine wanaoendelea kuitakangaza Tanzania katika Medali za Kimataifa nami nitazidi kuwapa ushirikiano pale panapowezekana ili tufike mbali nawatakia siku njema" Amesema Kumbilamoto.
Aidha katika hafla hiyo fupi ya kikabidhi vifaa hivyo vya mchezo wa ngumi, aliambatana na Uongozi wa Jumuiya wa Vijana Uvccm kata ya Vingunguti .
Katika hatua nyingine , alipata wasaa jioni ya Leo kuwatembelea Washindi wa nafasi ya Pili, katika Mashindano ya Mpira wa Miguu yaliyomalizika hivi karibuni ya Vingunguti Super Cup , Timu ya Watasu FM Mara baada ya Vijana hao kumpatia mwaliko.
Amesema lengo la kuanzishwa Mashindano hayo ndani ya kata yao ni pamoja na kukuza Mchezo wa Mpira wa Miguu kata ya Vingunguti ili kupata Vijana watakao weza kusaidia timu yetu ya Taifa kufanya vizuri Kimataifa.
" Mpira ni ajira, Ulaya wenzetu wanapiga hatua sana kutokana na mchezo huu, hivyo na sisi tukiupa uhai tutaleta mabadiliko chanya katika Soka la Tanzania na Kutengeneza maisha ya Vijana wetu" Ameongeza Kumbilamoto.
Amesema Mara baada ya kukabidhiwa kata hiyo kinachofuata ni kuona Sekta ya michezo katika Kata hiyo inapiga hatua kwa kuwezesha michezo yote kuanzia ngazi za Shule za Msingi, Sekondari na Mitaani.
Ametoa rai kwa Wazazi waunge mkono vipaji vya watoto zao kwani elimu inaendana na michezo.
Hata hivyo amesema Serikali ya awamu ya tano imetoa elimu bure hivyo lazima tuhakikishe watoto wetu wanafanya vizuri katika pande hizo mbili.
Amesema Ulaya watoto wanaingia katika mchezo wanaoupenda kutokana na ufaulu wa masomo yao ndio maana wanapiga hatua kubwa sana hivyo suala la michezo tulipe kipaumbele hususani mchezo wa Ngumi unaoonekana kutengwa Katika siku za hivi karibuni tofauti na mpira wa miguu.