DC MURO ATEMBELEA NA KUKAGUA UJENZI WA KITUO CHA AFYA MBUYUNI


Mkuu wa Wilaya ya Arumeru *Mh.Jerry Muro* amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Mbuyuni kilichopo katika Halmashauri ya Arusha Dc  ambacho Serikali imetenga fedha Milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Maabara na Nyumba ya Mtumishi wa kituo hicho pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yaliyokuwepo kwa lengo la kuwapa wananchi huduma bora za afya na kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

*Dc Muro* akikagua ujenzi wa Kituo hicho ameleza kuwa dhamira ya *Serikali ya Awamu ya Tano* ni kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya Afya kwa kuimarisha huduma za Afya na kujenga vituo vyenye hadhi vijijini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi hiyo ya Ujenzi wa Kituo hicho *Ndg.Leskara Olerangai* Ambaye pia ni Diwani mstaafu wa kata ya Oljoro ameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa  kuwezesha kutoa fedha kwa wakati huku akimpongeza *Dc Muro* kwa jitihada zake anazozifanya ili kuhakikisha ujenzi una kamilika kwa wakati.

*Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru*

*#ArumeruYe

Post a Comment

emo-but-icon

item