Bossou kurejea Yanga

Imebainika kuwa benchi la ufundi la Yanga lipo kwenye mchakato mkubwa wa kumrejesha aliyekuwa beki wao kisiki, Mtogo, Vincent Bossou kwenye usajili wa dirisha dogo ambapo tayari hivi karibuni mmoja wa viongozi alitumwa nchini Togo alipo mchezaji huyo kwa ajili ya kuongea naye ili waingie mkataba.
Yanga iliachana na Bossou mwanzoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake wa miaka miwili kufika ukingoni ambapo tangu muda huo beki huyo alirejea kwao Togo, ambapo sasa Yanga wanataka kumrejesha kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kuelekea katika michuano ya kimataifa.

Chanzo kutoka ndani ya Yanga kimesema kuwa  kiongozi huyo alienda Togo wiki iliyopita kwa ajili ya kuzungumza naye kwa ajili ya kumsainisha mkataba mpya ambao utamrejesha kwa mara nyingine beki huyo kwenye klabu hiyo.



“Kweli kuna kiongozi mmoja alienda kumfuata Bossou kule Togo kwa ajili ya kuzungumza naye kwa ajili ya kurejea tena kwetu, kwa sababu benchi la ufundi limeonyesha kumhitaji kwa ajili ya kuimarisha ulinzi zaidi. “Na tayari ameleta majibu kwamba yeye amekubali, kinachosubiriwa kwa sasa ni kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kisha yeye aje tumalizane naye, na hakuna ugumu juu yake kwa sababu kuna nafasi ya mchezaji mmoja wa kimataifa ipo wazi,” kilisema chanzo hicho.

 “Kweli Yanga wamekuja kuongea na mimi kwa ajili ya kunisajili, lakini nasikilizia wiki ijayo ndiyo nitajua kila kitu juu ya suala hilo. “Kwa sasa siwezi kuzungumzia sana lakini kila kitu kikikamilika ndipo nitazungumza, kwa sasa itambulike kama tetesi tu na kama unataka kujua zaidi ni bora ukawauliza viongozi wa Yanga na siyo mimi.”Alisema Bossou 


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online

Related

Kichuya gumzo Katavi

MASHABIKI wa Klabu ya Simba  waliomba kumuona Kichuya Katavi kwani ilikuwa ni  faida kwao kila walipomuona. Umaarufu wa Kichuya umezidi kupanda baada ya kufunga mabao katika mechi mbili ...

Ajibu awatuliza mzuka wana Yanga

Yanga imepata sare ya pili mfululizo huku mashabiki wake wakionyesha kutofurahishwa baada ya kikosi chao kuomba mechi iishe mapema wakati Singida United walipokuwa wakishambulia kama nyuki. Yang...

Morata ampagawisha Mourinho

Ligi kuu ya Uingereza na ilivyokuwa na matokeo ya jana kati ya Chelsea na Manchester United Manchester United: De Gea 7; Jones 5.5 (Fellaini 63, 5.5), Smalling 5, Bailly 5; Valencia 5, Matic ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:

item