DAS Ilala akoshwa na utendaji wa DC Mjema


















KATIBU Tawala wa Wilaya ya Ilala, Sheilla Edward Lukuba,  amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema,  kwa kumuita Mwalimu wa Watendaji Manispaa ya Ilala.

DAS Sheilla , amesema DC Mjema ni mfano wa kuigwa kwani amekuwa akijitoa kuhakikisha kero za wananchi zinatatuliwa.

Amesema katika utendaji wake wa kazi tangia ateuliwe kushika nyadhifa hiyo hajawahi kuona mkuu wa wilaya mchapakazi mwenye  uchu wa maendeleo katika Wilaya yake.

Amesema tangia mwaka 2003 aanze kazi ya Uhasibu mpaka Leo DC Mjema atabakia kuwa Mwalimu wake kwa kuwa ni Mtendaji asiye na makuu.

 Aidha amewataka Wananchi wa Wilaya ya Ilala kutoa ushirikiano kwa Viongozi wao Katika kuwaletea maendeleo.

" Kwanza napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mkuu wa Wilaya Mh: Sophia Mjema, kwakweli huyu mama anafanya kazi kweli na amekuwa kiongozi  shupavu kwani kutembelea kata zote 36 Wilaya ya Ilala sio kazi ndogo, hivyo kila Mtendaji anapaswa kuendana na kasi ya DC wetu ili tupunguze changamoto na kero za wananchi kwa kuzifanyia kazi kwa vitendo" Amesema DAS Sheila.

Hata hivyo , amewataka Watendaji wote kuacha kukaa Ofisini na badala yake washuke chini kuwasikiliza wananchi wanasemaje na wa nataka nini katika Serikali yao ambayo ni sikivu na tulivu yenye lengo la  kuwapigania wanyonge na umumasikini.

Ameupongeza Uongozi wote wa Manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Mkurugenzi kwa jinsi walivyoonyesha ushirikiano kutatua kero kwa asilimia kubwa katika kuwaaminisha wananchi kwamba Serikali yao ni Serikali ya kazi kweli.

 Mbali na hayo, amesema kila Mtendaji akifanya jukumu lake ipasavyo basi hii migogoro inayojitokeza kwa wingi itapungua na wananchi watazidi kuipenda Serikali yao inayoongozwa kwa kufuata Ilani ya Chama cha Mapinduzi ( CCM)  chini ya Rais Dtk John Pombe Magufuli.

Amesema DC Mjema yupo  kwa ajili ya wana Ilala hivyo mtu  au watu wenye  kero zao wanaombwa kufika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya kwa ajili ya kupatiwa huduma bila kujali Dini, Ukabila na Uchama kwa kuwa maendeleo hayana Chama.


Amesema Serikali ya Rais Magufuli inatumikia Watanzania wote lengo ni kuona nchi hii inafikia kwenye Uchumi wa kati wa Tanzania ya Viwanda.

Post a Comment

emo-but-icon

item