DC Mjema awataka Viongozi wa Soko la Samaki Feri kuwajibika

MKUU wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, ameutaka  Uongozi wa Soko la  Feri Kivukoni kuwajibika ili kuondokana na changamoto. Hayo ameyasema Leo Mara baada ya kukagua Zone zote zilizopo katika Soko hilo. Akizungumza na Waandishi wa Habari leo, ikiwa  ni ziara yake ya jutembelea majimbo yote ndani ya Manispaa ya Ilala ambapo Leo ametembelea Jumbo la  Ilala.

Dc Mjema, amesema katika zone hizo amegundua yapo mapungu yanayotokana na Manispaa lakini kubwa zaidi ni muuingiliano wa Biashara unaofanyika katika Soko hilo.

Amesema viongozi wawe na utaratibu wa kuwafikia watu wao na sio kungoja mpaka yeye afanye ziara, hivyo amesema kero ambazo zitakuwa ndani ya uwezo wao atazifanyia kazi na zilizo nje atazifikisha Katika Wizara husika.

Amesema kazi ya Viongozi ni kuwatumikia watu wanyonge , hivyo Serikali ya awamu ya tano  haitawavumilia Watendaji wazembe. Aidha amesema Soko hilo linakabiliwa na changamoto mbali mbali, miongoni Mwa changamoto hizo ni pamoja na ubovu wa miundombinu, vyoo , umeme , Maji n.k.

 Kuhusu swala la  ukosefu wa vyoo, amesema tayari wameingiza katika bajeti ya kujenga Vyoo 18 katika Zone 8 na Vyoo 24 katika Zone Namba 3. Akitolea ufafanuzi juu  ya Vizimba kutokuwa na Namba, amesema wapo katika mpango wa kuweka Namba za kisasa baada ya hatua ya ukarabati kufanyika katika Soko hilo.

 Katika kutatua kero ya Umeme, amemuagiza Injinia kukagua mifumo ya umeme ili kuboresha huduma hizo ikiwamo uwekaji wa Taa.

" Najua Soko hili linachangamoto nyingi ambazo zinachangiwa na Manispaa lakini zaidi kutowajibika kwa viongozi wanaotaka kujinufaisha matumbo yao, Mimi nimepokea hizo Changamoto nitazifanyia kazi kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi Manispaa " Amesema Dc Mjema.

Hata hivyo ilijitokeza suala la usimamishwaji wa uvuvi wa Kambamti  kutokana na utafiti wa Kisayansi uliofanywa kwamba  kuna uhaba wa kambamti hivyo Wizara ilitoa muda wa miezi 7 ili kuongezeka kwa kambamti na kuemdelea na shughuli za uvuvi.

 Katika kuona suala hilo linafahamika na wengi  katika kujiridhisha sababu zilizotolewa na Wizara, Dc Mjema, amewataka wafanya Biashara hiyo wachaguane watu 5 ili awaunganishe na Wizara na baada ya kupata elimu hiyo waitoe kwa wenzao.Amesema Tarehe 25 Oktoba, atarudi tena ili kuona matatizo yanayotokea Zone Namba 3 na Zone namba 1 yanatatulika.

Amesema Biashara ya Samaki kwa Sasa iendelee kama utaratibu unavyosema ili kuepuka kuingilia kwa Biashara na kila Zone ifanye kazi zake. Katika kutatua kero ya Biashara ya hotel inayifanyika Zone Namba 4 ambapo inasemekana kuna utata kuhusu mmiliki na mwendeshaji, amemtaka Katibu Tawala kushughulikia suala hilo kwa kumuitaa ofisini mmiliki wa Hoteli hiyo.

 Katika hatua nyingine, Dc Mjema ametembelea Zone Namba 5 na kukutana na tatizo la  umeme la  kutozwa bei  kubwa lakini amesema watazungumza na Manispaa kuhakikisha kila kizumba kinakuwa na mita zake ili kupunguza gharama na ghadhabu ya uchangishaji umeme jambo linaloleta sintofahamu ya kujua Fulani ametumia kipi na anatakiwa achange kipi.

 Mbali na hayo kero nyingine ilikuwa  ni ya baadhi ya Wafanyabiashara kufanya Biashara nje ya geti ambayo ni sawa na Biashara inayofanywa ndani jambo ambalo limelalamikiwa kukandamiza wafanya Biashara wa ndani kutopata mapato na kushondwa kulipa mikopo. Hivyo amemuagiza Afisa Mtendaji Kata ya Kivukoni kuhakikisha hakuna wafanya Biashara nje  ya geti.

Kuhusu tuhuma za Mwenyekiti kutokuitisha vikao, DC Mjema amemtaka Afisa Ushirika kufika kesho Oktoba 16 kwa ajili ya kutatua hizo changamoto zao. Amesema mageti yote kuanzia Leo yawe wazi na kuhusu huduma za Choo wafanya Biashara wote wenye namba  watoe tozo ya Shilingi 200 kwa siku.

katika kuona suala hilo linafahamika na wengi  katika kujiridhisha sababu zilizotolewa na Wizara, Dc Mjema, amewataka wafanya Biashara hiyo wachaguane watu 5 ili awaunganishe na Wizara na baada ya kupata elimu hiyo waitoe kwa wenzao.

Amesema Tarehe 25 Oktoba, atarudi tena ili kuona matatizo yanayotokea Zone Namba 3 na Zone namba 1 yanatatulika.

Amesema Biashara ya Samaki kwa Sasa iendelee kama utaratibu unavyosema ili kuepuka kuingilia kwa Biashara na kila Zone ifanye kazi zake. Katika kutatua kero ya Biashara ya hotel inayifanyika Zone Namba 4 ambapo inasemekana kuna utata kuhusu mmiliki na mwendeshaji, amemtaka Katibu Tawala kushughulikia suala hilo kwa kumuitaa ofisini mmiliki wa Hoteli hiyo.

Katika hatua nyingine, Dc Mjema ametembelea Zone Namba 5 na kukutana na tatizo la  umeme la  kutozwa bei  kubwa lakini amesema watazungumza na Manispaa kuhakikisha kila kizumba kinakuwa na mita zake ili kupunguza gharama na ghadhabu ya uchangishaji umeme jambo linaloleta sintofahamu ya kujua Fulani ametumia kipi na anatakiwa achange kipi.

 Mbali na hayo kero nyingine ilikuwa  ni ya baadhi ya Wafanyabiashara kufanya Biashara nje ya geti ambayo ni sawa na Biashara inayofanywa ndani jambo ambalo limelalamikiwa kukandamiza wafanya Biashara wa ndani kutopata mapato na kushondwa kulipa mikopo. Hivyo amemuagiza Afisa Mtendaji Kata ya Kivukoni kuhakikisha hakuna wafanya Biashara nje  ya geti.

Kuhusu tuhuma za Mwenyekiti kutokuitisha vikao, DC Mjema amemtaka Afisa Ushirika kufika kesho Oktoba 16 kwa ajili ya kutatua hizo changamoto zao. Amesema mageti yote kuanzia Leo yawe wazi na kuhusu huduma za Choo wafanya Biashara wote wenye namba  watoe tozo ya Shilingi 200 kwa siku.

Post a Comment

emo-but-icon

item