DC Mjema atoa agizo wafanya Biashara pembezoni Mwa bara bara kwenda maeneo waliyopangiwa


 Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amewataka watu wote wanaofanya  Biashara pembezoni Mwa bara bara waondoke na kwenda Katika maeneo waliyopangiwa.

DC Mjema, ameyasema hayo katika ziara yake ya kuzunguka katika Soko la  Kisutu  Leo. Aidha amesema wafanya Biashara hao wanafanya Biashara kinyume na Sheria hivyo ni lazima wafuate utaratibu wakwenda  maeneo tengwa.

Miongoni Mwa wafanya Biashara hao ni pamoja na Wauza matunda, Nguo ,viatu na wale wanaouza mboga mboga. Amesema wafanya Biashara hao wanahitaji kutambulika na Serikali kitendo cha wao kujificha ficha kinawakosesha fursa za kufikia malengo na kutoaminika.

 Amesema tayari wameshatenga maeneo ya muda ambayo yatatumiwa na wafanya Biashara hao huku wakisubiria ujenzi wa Soko jipya la  kisasa la  Kisutu kukamilika .

" Serikali chini ya Rais Magufuli ilitoa maagizo kwamba  hatuwezi kuwahamisha kabla hatujapata maeneo, Mimi nimeshapata Sasa kilichobakia muhame kuondoa kero kwani Barbara ni kwa ajili ya watembea kwa miguu, nawapa wiki moja Afisa Mtendaji awaandikishe kwa wale wasioandikishwa ili muondoke na kuelekea kona ya Soko la  Kisutu " Amesema DC Mjema.

 Amesema miongoni Mwa faida watakazo zipata wafanya Biashara hao ni pamoja na kutambulika, kupata vitambulisho vya Taifa, vya kazi na kukopesheka kwenye taasisi za kifedha kama vile Benki ili kujiendeleza kiuchumi katika kufikia uchumi wa kati.

 Kuhusu tuhuma za uuzwaji wa maeneo, DC Mjema, amemtaka OCD Manispaa ya Ilala kufuatilia wahusika ambao ni Parking System ili kujua ukweli wa jambo hilo na wakigundulika wafikishwe Mahakamani.

Pia wale wote wanaojihusisha na uuzaji wa maeneo ya wazi Barabarani wakamatwe. Kuhusu tuhuma za ukamataji wa boda boda , DC Mjema , amesema wameanzisha semina kwa madereva wa boda boda zitakazowafanya kujua Sheria. Mbali na hayo, DC Mjema, amesema wale wenye  Gereji bubu atawatafutia maeneo yaliyo salama na utulivu.

 Amesema dhumuni la  Serikali  sio kuwakimbiza Bali ni kuwawekea maeneo salama  na kutambulika kwa kupatiwa vitambulisho.

 Katika kuhitimisha ziara hiyo katika Mtaa wa Mchafu Koge, amesema lazima Viongozi waungane na wananchi kuanzia ngazi zote wakifanya hivyo watapunguza kero kwa asilimia kubwa.

Post a Comment

emo-but-icon

item