DC Mjema afungua mradi wa vyoo vya kisasa vyenye thamani ya Shilingi Milioni 62 Shule ya Msingi Bunge







Jumla ya Shilingi Milioni 62 yatumika ujengaji vyoo vya kisasa Shule ya Msingi Bunge. KATIKA kuona Wanafunzi wanakuwa na huduma nzuri ya vyoo , Shule ya Msingi Bunge iluyopo Mkoa wa Dar es Salam,imekuwa miongoni Mwa Shule zilizopata huduma hiyo ukiwa ni mpango wa Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema, kuhakikisha watoto wakike wanapatiwa vyoo. Katika hatua hiyo, Jumla ya Shilingi Milioni 62 zimetumika kujenga vyoo hivyo vyenye jumla ya matundu 16.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mara baada ya uzinduzi huo, Dc Mjema, amewapongeza Manispaa ya Ilala pamoja na  wadau mbali mbali waliofanikisha mradi huo. Aidha , DC Mjema, amesema mpaka Sasa mpango wa kujenga vyoo vya Mtoto wa kike umefanikiwa kujenga Vyoo 5 katika Shule tano  ndani ya Manispaa ya Ilala.

Pia DC Mjema, amesema katika Ujenzi huo wa vyoo, ni moja ya mikakati ya kumuunga Mkono Rais John Magufuli ya kutoa elimu Bure.

"  Tuna imani na Serikali ya awamu ya tano, hivyo sisi kama wasaidizi wake tunafanya Yale anayoyataka kwa kuwatumikia wananchi na kuona suala La elimu bure linakuwa na faida  kwa Watanzania wote" Amesema Dc Mjema.

Katika hatua nyingine , Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Radhia Mfalingundi, amesema jumla ya mashimo katika vyoo hivyo ni 16 ambapo  wanaume vyoo 8 na Wanawake vyoo 8. Amesema awali walikuwa na Matundu 10 upande wa  Wavulana na matundu 13.

 Pia amesema Shule hiyo ina  Wanafunzi 2264, Wavulana 1207 na Wasicha 1067. Hata hivyo Mwalimu huyo amesema Shule yao inakabiliwa na Changamoto  ya uchakavu wa Majengo  maana Majengo  yaliyopo ni ya zamani .

Post a Comment

emo-but-icon

item