ZIARA YA DC MJEMA, CHANGAMOTO YA ULINZI YAJITOKEZA KILA KONA
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/08/ziara-ya-dc-mjema-changamoto-ya-ulinzi.html
WAKATI ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Illa, Sophia Mjema, ikiwa
imemalizika mara baada ya kutembelea baadhi ya miradi ya wananchi kwenye Jimbo
la Ukonga, changamoto nyingi zilijitokeza lakini kubwa zaidi ni la ulinzi na
usalama ambalo lilijitokeza kila kona.

Katika ziara izo, jumla ya Kata 13, zilitemebelewa ambapo
kila kata kuiuwa na kikao cha mjuuisho wa wananchi kuelezea kero zao huku
wakazi wengi wakiwa na shauku ya kutaka kujua ni lini watanifaika na miradi yao
kwa ujumla.
Mkuu wa wilaya ya Ilala, katika ziara zake zote, suala la
ulinzi na usalama liijitokeza kila kona, huku maagizo aliyoyatoa yakionekna
kuwapa moyo na kuwatia faraja sana wakazi wengi waliojitokeza kwenye ziara
hizo.
Akizungumza na waaanishi wa habari, jana kwenye ziara ya
Kata ya Msongola na Chanika, DC Mjema,
alisema kuwa , suala la ulinzi ni la kil mtu licha ya kuonekana kupewa jukumu
kubwa Askari.
Alisema kuwa, kama kuna wakazi wanawajua waharifu hao,
wanatakiwa kushirikiana na viongozi wao wa Kata na Serkali za Mitaa ili suala
hlo lipatiwe ufumbuzi wa haraka na kuhakikisha hali ya usalama ina kuwa shwari
.
”Nimesikia kwamba wapo boda boda wanaokabwa, wengine
wanauwawa na mnasema hamuwafahau, nitoe rai kwa wazazi, wakina baba na wakina
mama, kama unamtoto wako unajua anajiuisha na ujambazi, kibaka, mkanye mara
moja kwani tukimkamata sisi tutampiga sana, hivyo ni wajibu wenu kujilinda
wenyewe na kuchunguzana”Alisema DC Mjema.
Akijibu hoja za wananchi kuhusu vijana wao wanaojihusihsa na
boda boda kukamatwa na polisi wakidai
wanaonewa, DC Mjema alisema inaweza kuwa kweli wanaonewa na wengine wanakutwa
na hatia, hivyo ametaka Jeshi la Polisi kanda ya Ukonga wanapowakamata watu wasio na hatia wawaachie
huru huku wenye makosa wapigwe sana.
Aidha, katika ziara hiyo ya jana, DC Mjema, alifanikiwa
kutembelea mradi wa Zahanati ya Mtaa wa
Ruhanga, uliopo Kata ya Msongola wenye juma ya Vyumba 12 ambao unategemea kumalizika
mwaka huu Oktoba wenye thamani ya shilingi Milioni 123 utakao hudumia jumla ya mitaa miwili ikiwamo Kiboga
na Ruhanga.
Mbali na mrai wa Zahanati, pia alitembelea mradi wa Kisima Mtaa
wa Mkera Kata ya Msngola, ambapo kisima hicho kina jumla ya Mita 150, takao
hudumumia watu 1500 sawa na mita 5000 ambao una DP 3 katika mitaa 2, mnara
mmoja upo shule na mwengine utaudumia
jamii na ukamilikaji wake unatarajiwa kuwa 30/10/2018
Katika hitimisho la ziara yake, pia alitembelea Kata ya
Chanika na kufanikiwa kukutana na wananchi ambao walitoa kero zao na kuahidi
kuzifanyia kazi na nyingine akizitatua papo kwa papo .
Miongoni mwa miradi ambayo alitemebelea Chanika ni pamoja na
mradi mkubwa wa Stendi ya Mabasi, miradi
ya Elimu, Afya pamoja na Ulinzi na usalama na soko.