Kumbilamoto atoa neno mazishi ya Msanii Bagamoyo


NAIBU Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwanini wa Kata ya Vingunguti, Mh: Omary Kumbilamoto, ametoa neno kwenye mazishi    ya Msanii Nguli wa Filamu hapa Nchini na Mlezi wa Wasanii, Kassim Taalib,yaliyofanyika Wilaya ya Bagamoyo Jumapili  Mkoani Pwani.
Akizungumza na Waandishi wa habari  leo  mara baada ya kumalizika kwa mazishi hayo, Kumbilamoto amesema Kassim Taalib , licha ya kuwa msanii wa Filamu pia alikuwa kiongozi bora wa kuwalea Wasanii kimaadili na kuwafundisha nguzo za Sanaa ili kukuza vipaji vyao.
Amesema kuwa wamepoteza mtu muhimu sana katika Jamii hususani katika Tasnia ya Sanaa hapa nchini, huku akisema Taalib katika uhai wake alikuwa akipenda kushirikiana na kila Msanii bila ya kuwatenga na ubaguzi wa aina yoyote.

""Marehemu Taalib mbali na kuwa msanii , alikuwa mshauri wangu , baba mlezi ukiangalaia asilimia kubwa ya Wasanii  nguli hapa nchini walipitia katika mikono yake, tunacha kujifunza kwa Wasanii waliobakia waige mfano wa Maisha ya baba yetu Mzee Kassim Taalib, mwisho napenda kusema Mungu ajalie kaburi lake liwe kiwanja cha pepo amin""Almesema  Kumbilamoto.

Ikumbukwe kwamba Marehemu mbali na Sanaa alikuwa anamchango mkubwa wa kukuza Elimu ya Tanzania, kwani mpaka umauti unamkuta ameacha Shule inayojulikana kwa jina la Splendid iliyopo Ilala Bunguni Jijini Dar es Salaam.

Mazsihi ya Marehemu Taalib yalihuzuliwa na baadhi ya Wasanii nguli hapa nchini wamejitokeza kwa wingi katika safari yake ya mwisho , akiwemo Dude, Dk Cheni  na wenzake.

Related

habari 5299557101576395275

Post a Comment

emo-but-icon

item