KUMBILAMOTO AFUNGUA KAMPENI KIBABE, MAMIA WAJITOKEZA KUMRAKI
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/08/kumbilamoto-afungua-kampeni-kibabe.html

ALIYEKUWA Diwani wa Kata ya Vingunguti na Naibu Meya wa
Manispaa ya Ilala, Mh:Omary Said Kumbilamoto, jana amefungua kampeni yake ya
kwanza tangia ateuliwe na chama chake kipya cha CCM hii ni mara baada ya
Kujihudhuru nyadhifa zake zote kuptia tiketi ya Chama cha CUF na kujiunga Chama cha Mapinduzi (CCM ).


Katika kuonyesha Kumbilamoto bado anapendwa na Wananchi
wake, tulishuhudia Mamia ya watu
wakifurika Kwenye Uwanja wa Msikate Tamaa uliopo Nyuma ya Zahahnati ya
Vingunguti na kushuhudia baadhi ya Viongozi wa Ngazi za Juu ya Chama Cha
Mapinduzi wakiongozana na Mh Kumbilamoto hii yote ni kuona Kata hiyo inarudi
katika mikono yao.
Miongoni mwa Viongozi wa Juu wa Chama cha Mapinduzi
waliohudhuria Ufunguzi huo wa Kampeni ni pamoja na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James ambaye
alikuwa Mgeni Rasmi, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam ,Mh: Kate Kamba, Katibu
Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Simon Mwakifwamba , Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala ,Joyce Mkagaula, Bonnah Kaluwa Mbunge
wa Jimbo la Ukonga , na baadhi ya Makada wakubwa waliotoka Chama cha Upinzani aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro Ndugu Emannuel Mlaki na Viongozi wengine wa ngazi mbali mbali
katika Mkoa wa Dar es Salaam na Wialaya zote.
Aidha katika uzinduzi huo, Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Kheri James, aliwataka Wakazi wa Vingunguti wasifanye makosa na kumchagua Omary
Kumbilamoto ili azidi kuwatumikia wananchi wa Kata hiyo kwa kuwa Ilani ya CCM
inatekelezeka ikiongozwa na Rais John Pombe Magufuli na wasaidizi wake katika
ngazi mbali mbali.
Alisema kuwa wawapuuze wapinzania amabao kazi yao ni
kupandikiza chuku dhidi ya Viongozi na Taiafa lao kwa Mabepari wa Ulaya jambo
ambalo ni hatari sana na hawatalimezea mate
ili kuendelea kuimarisha nchi na Maendeleo kwa Wananchi wake
waliyokiamini Chama cha Mapinduzi (CCM).
“Wapinzani wao wanapinga kila jambo katika nchi hii, liwe
zuri liwe baya , sasa wanatupa mashaka sana utasema wao si Watanzania kila
jambo wanalipeleka Ulaya, kwani Serikali
yao haiwezi kuwasikiliza? Kiukweli lazima tukemee hili jambo na kamwe tusiwape
madaraka watatupeleka motoni, tunahitaji Viongozi wenye busara na wachapa kazi
kama ilivyo Kumbilamoto , hivyo wakazi wa Vingunguti tusifanye makosa siku ya
kupiga kura tuhakikishe tunashinda kwa kishindo kikubwa na kumrudisha tena
Kumbilamoto kuwa Diwani akawatumikie kiufasaha maana anajua shida zenu na
mmetoka nae mbali sana”Alisema Kheri James
Katika hatua nyingine, Mgombea kiti hicho cha Diwani, Mh:
Kumbilamoto , aliwaeleza wakazi wa Vingunguti walichokivuna kipindi yupo Diwani
na matarajio yake ya kuendeleza yale aliyoyaacha katika kuijenga Vingunguti
Mpya.


Pia Kumbilamoto alisema kitu kilichompelekea kujihuzuru nyadhifa
zake ndani ya CUF ni kutokana na Mgogoro unaoendelea ndani ya CUF pamoja na
Baadhi ya Viongozi wa Chama hicho kumshtumu kufanya kazi bega kwa began a Viongozi
wa Serikali jambo ambalo kwa upande wake aliona halipo sawa.


“ Mimi ni mwanadamu najitambua, ili kufikia mafanikio ni
lazima Viongozi wa Serikali wahusishwe kwakuwa wao wapo Madarakani , sasa
wenzangu jambo hili hawalitaki kabisa, utaona maajabu kipindi tunapata Mafuriko
Vingunguti hakuna hata Kiongozi mmoja wa CUF aliyejitokeza zaidi Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Paul Makonda na Mkuu wa Wialya ya Ilala Dada yangu Sophia
Mjema ndio walinisaidia, sasa kwa hali hii kweli utasema unabakia Kung’ang’ania CUF, ndugu zangu naombeni mnipokee, kazi
zangu mmeziona na nitazidi kuwasaidia bila ubaguzi wa aina yoyote kwa maslahi
ya Wana Vingunguti”Alisema Kumbilamoto
Katika kuelekea tamati ya kufunga Kmapeni tulishuhudia
baadhi ya Viongozi na makada wa Chama cha CUF wakijiunga na CCM wakimfuata
Diwani wao wengi wao wakisema Chama chao kimekufa hivyo CCM ndiyo chama pekee
chenye kutekeleza Sera zao kwa Vitendo.
Miongoni mwa wananchama waliorudisha kadi ni pamoja na Salma
Emannuel, Mjumbe wa Kmati Tendaji ya Kata CUF, Adam Omary, Mwenyekiti wa Boda
Boda upande wa CUF, Maulidi Mfunga Mwenyekiti wa Tawi la Mtambani tiketi ya
CUF.
Uzinduzi huo uliambatana na Bendi ya Wasanii kutoka First Class Modern Taarabu chini ya Amigo ambao walitumbuiza vizuri wakiwa na nyimbo maalumu ya kumsifu Mh: Omary Kumbilamoto
Kmapeni hizo zitaendelea tena kwenye Uwanja wa Msikate Tamaa, nyuma ya Zahanati ya Vingunguti, Siku ya Jumatano ya Tarehe 29 majira ya Saa 9 Mchana .
Kmapeni hizo zitaendelea tena kwenye Uwanja wa Msikate Tamaa, nyuma ya Zahanati ya Vingunguti, Siku ya Jumatano ya Tarehe 29 majira ya Saa 9 Mchana .
![]() |
| Mh: Omary Kumbilamoto akiwa na Mkewe Mama Kumbilamoto mara baada ya kukamilika kwa kampeni jana |











