KUMBILAMOTO AZIDI KUCHANJA MBUGA , KAMPENI ZAKE ZAWA GUMZO KILA KONA.




MGOMBEA nafasi ya Diwani kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Omary Said Kumbilamoto leo ameendelea na Kampeni yake ya pili kwenye hadhara ya Eneo la Mtaa wa Butiama Kata ya Vingunguti katika kunadi sera zake kuelekea uchaguzi mdogo wa marudio.

Kumbilamoto ambaye alikuwa Diwani wa Zamani wa Kata hiyo kupitia CUF, amesema yeye kwa sasa sio mpiga kelele bali Wananchi wa Vingunguti wanafahamu uwezo wake na uwajibikaji kwa Wakazi hao.

Amesema kuwa, moja ya mikakati amabyo ataifanya katika Sekta ya Usafiri ni pamoja na Kuhakikisha Magari yanafika Katika Mtaa wa Butiama kwani mpaka sasa mazungumzo na Mkurugenzi wa Mashkof yalishafanika kinachosubiriwa ni kuonana na Mkuu wa Wilaya ya Ilalla pamoja na SUMATRA wakae meza moja wakubaliane ili kuondoa adha wanazozipata wananchi wa Mtaa huo.

Katika Upande wa Afya , amesema kuwa tayari ahadi zote alizozitoa kashazipatia majawabu hivyo hana deni tena kilichobakia ni kero za Shule pamoja na Maji ambapo amewahidi wakimchagua wakazi wa Mtaa wa Butiama watapata maji masaa Ishirini na nne.

Hata hivyo, amesema kuwa, Wageni wengi wanaingia Dar es Salaam wakifika wakitafuta nyama weni wao wamekuwa wakiagiza kutoka Mikoa mingine, hivyo amesema Serikali tayari ishatenga pesa za Kujenga Chinjio la kisasa litakalo kuwa likichinja kuanzia Ngo’mbe 1000 kwa siku jambo ambalo litasaidia kuingiza pato Serikalini na Kata yake .
Mbali na ahadi hizo, amewahakikishia Polisi walopo kata yake kuwapelekea TV kubwa (Flat Screen) pamoja na King’amuzi cha Azam TV ili wazidi kuona mazuri yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli.
Pia,  amewaomba Wananchi waendelee kuwa na imai nay eye kwani ana mategemeo makubwa ya kuifikisha Vingunguti mbali na kuwaambia wawapuuze Wapinzania wanaoleta Propaganda dhidi yake.

“Nipende kusema kuwa , mimi nawafahamu sana najua changamoto zenu zipo wapi, nilichelewa kufanikisha kwa kuwa Chama nilichokuwa nacho mwanzo hakikutaka kushiriiana na Serikali, sasa niwaombe radhi nmekuja nyumba kubwa tutatekeleza kwa vitendo yale yote niliyo yaahidi na kukwama kwa kushirikiana na Wananchi wangu”Amesema Kumbilamoto


Ikumbukwe kwamba huu ni mkutano wa pili kuzinuliwa ambapo mkutano wa kwanza ulifanyika Uwanja wa Msikate tama ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenyeiti wa UVCCM Taifa, Kheri James na mkutano wa leo mgeni Rasmi ni Mwenyekiti wa Wazazi CCM Mkoa wa Dar es Salaam , Ndugu Frank Kamugisha 

Mkutano mwengine utaendelea mpaka ratiba itakapo tolewa, na Uchguzi utafanyika Mwezi wa 9/16/2018 na siku ya Kufunga Kampeni ni Tarehe 15/9/2018.

Related

SIASA 304126678732814652

Post a Comment

emo-but-icon

item