Taxify yazindua huduma wezeshi kwa Wateja wake Dodoma
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/09/taxify-yazindua-huduma-wezeshi-kwa.html
Huduma ya teknologia ya teksi inayoongoza Ulaya na Afrika ya Taxify leo imezinduliwa jijini Dodoma na mamia ya madereva teksi ambao wamesajiliwa na Taxify wameanza kutoa huduma kwa wananchi.
Huduma ya Taxify mjini Dodoma itatoa njia salama na ya bei nafuu kwa abiria kupata usafarishaji na usalama wa wateja umeongezeka kwa kutumia teknolojia ya “Share your ETA“ ambayo inampatia mteja fursa ya kutaarifu familia na marafiki safari yake na kuwahakikishia usalama wake.
Menjea Mkuu Tanzania Bw. Remmy Eseka amesema: "Baada ya kuzindua huduma yetu jijini Dar es Salaam na Mwanza, tunaendelea kupanua wigo wa huduma, na mji mkuu wa Dodoma ni mojawapo ya miji ya msingi katika soko letu. Tuna imani ya kwamba watanzania watanufaika na huduma zetu.”
KAMPUNI inayojishughulisha na Huduma rahisi za Usafiri kwa Wateja, Taxify, leo imezindua Ofa mbali mbali katika Jiji la Dodoma zikilenga kunufaisha Madereva ambao wamesajiliwa kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Kampuni imefanikiwa kutoa mikopo ya simu za kisasa za kiganjani ambazo zitawawezesha Maereva kujiunga pamoja na kutumia Teknolojia hiyo ya kisasa katika kuwahudumia Wateja.
Katika kuona wanaboresha mfumo wa malipo kwa Madereva, wamewataka wale wote waliosajiliwa katika mfumo huo walipe pesa kwa awamu ya mwezi kwa mwezi na faida kaika faia watakayopata kwenye biashara zao.
Katika kutanua wigo wa Biashara, Kampuni hiyo kwa kushiriiana na Kampuni ya Mafuta ya Total, imetoa ahdi ya punguzo la Bei ya mafuta na bidhaa za Total kwa Madereva wote ambao watajiunga na kadi ya Total.
"Hii ni furaha kubwa sana ya kuwa watu wa kwanza kutoa huduma ya Teknologia ya texsi mjini Dodoma na kuunganisha madereva mbalimbali na huduma yetu. Tuna uhakika teknologia yetu italeta urahisi na kupunguza ucheleshewaji wa kutoa huduma katika Jiji,”* amesema Shivachi Muleji, Meneja Mkuu wa Afrika Mashariki.
Aidha, Kampuni hiyo imelenga kuwanufaisha madereva kwa kutoza ada ndogo ya kutumia Teknologia yao kwa asilimia 15% tu, ambayo ni zaidi ya nusu ya ada wa washindani wao nchini na kote Duniani.
"Siku zote katika kuona tunanufaika, huwa tunakuja na mbinu mbali mbali katika ushirikiano katika kuwapatia fursa Madereva ambazo zitamwezesha kupata faida kubwa zaidi katika upunguzaji wa gharama za kufanya biashara, ni imani yetu kwamba Madereva pamoja na Wateja watafurahia kazi zetu na kuwarahishsia madereva kutoa huduma bora kwa Wateja, mpaka sasa Madereva wetu wamefurahishwa na punguzo la gharama ya mafuta kwa kuwa punguzo ni hapo kwa papo kwenye pampu"Amesema Remmy Eseka.
Kampuni ya taxify imeweka mipango ya kupanua wigo wa huduma katika Afrika Mashariki na inayomikakati ya kuleta huduma yao kwa madereva bajaji na pikipiki.
