Makonda kuja na mwarobaini wa uchafu dar es salaam
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/06/makonda-kuja-na-mwarobaini-wa-uchafu.html

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana Paul Makonda amekili kuwa jiji lake ni chafu hivyo ameandaa mkakati wa kuhakikisha jiji hilo linakuwa safi kama majiji mengine inchini ambayo yanasifika kwa usafi ikiwemo Moshi.
Hayo amesema wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira amesema kuwa mazingira ya jiji la Dar es salaam ni machafu na hayendani na wakazi wanaoishi katika jiji hilo
kwa kuliona hilo ameamua kuwa na mpango wa kuanza kampeni yakuhamasisha usafi wa mazingira kwani wananchi wamekua na tabia ya kufunga maduka siku ya jumamosi kwa kisingizio cha kufanya usafi kama ilivyotakiwa hivyo amehaidi kutafuta mwarobaini wa kulimaliza tatizo hilo
oparesheni ya usafi wa mazingira kwa mkoa wa Dar es salaam inatarajiwa kuanza julai mosi na kudumu kwa kipindi cha mwezi mmoja huku akitoa rai ya kutomuogopa mtu na kutaka sheria isimamiwe