kumbilamoto awaomba radhi watumiaji wa barabara ya kata yake
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/06/kumbilamoto-awaomba-radhi-watumiaji-wa.html

Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Kumbilamoto amewaomba radhi watumiaji wa barabara ya vingunguti hasa wenye magari kwa uharibifu walioupata kutokana na ubovu wa barabara ya Vingunguti mnyamani na barabara kubwa ya machinjioni.
Akizungumza na Raia Tanzania, a Jijini Dar es salaam akiwa kwenye matengenezo ya barabara hiyo ameeleza kuwa jukumu la kujenga barabara sio la manispaa ya ilala ni la TARULA chombo ambacho kimeundwa na serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu ya barabara
Aidha Kumbilamoto ameongeza kuwa kazi ya manispaa zote Tanzania ni kupeleka pesa katika Akaunti ya TARULA na wao ndio wanajukumu la kuamua kuanza na barabara ipi wajenge na si madiwani kama wananchi wanavyojua na kuwatupia lawama watendaji.
Hata hivyo amesema kuwa anashukuru kwa ushirikiano wanaouonyesha wanainchi wa kata yake kwa kuhakikisha kuwa wanatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili bila kutegema zaidi serikali kuwafanyia.
“Asie shukuru kwa kidogo hata akipewa kikubwa hawezi kushukuru nitoe shukrani za dhati kwa Vijana wa Vingunguti walojitolea kushirikiana nami katika kufukia mashimo katika barabara kubwa ya machinjioni”