Serikali nisaidieni kwa ukatili niliofanyiwa: Emijidius Cornel

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/serikali-nisaidieni-kwa-ukatili.html

KATIKA hali isyo ya kawadia Kijana Emijidius Cornel Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo cha Elimu cha DUCE, amejikuta akifanyiwa vitendo vya kinyama na Walinzi wa Chuo hicho mara baada ya kumpiga na kumsababishaia kupelekwa Hospitali


Akizungumza na waandishi wa habari, amesema nkitendo alichofanyiwa kilichotokea Mei 5 mwaka huu, hakufurahsihwa nacho kwani ameviiita vya unyanyasaji na ukatili uliopitiliza huku lawama zake zikienda kwa Uongozi wa Chuo ambao ulikaa kimya bila kuchukua hatua zozote mpaka anatolewa Hospitalini ambapo alilazwa kwa muda wa siku 20 kwenye wodi ya wagonjwa wanaougua Ugonjwa wa Akili.

Amesema kuwa mara baada ya kupigwa na Waalinzi hao, alienda kukata PF3 kwa ajili ya matibabu ndipo Uongozi wa Duce kwa kushirikiana na Daktari wa Zahanati ya chuo kumchukua kijana huyo katika Gari la wagonjwa na kumfikisha Hospitali ya Temeke kwa ajili ya matibabu.
lakini amesema kuwa, ameshangazwa na kitendo cha daktari huyo kuingilia mamlaka ya watu wengine mara baada ya kumtaka kijana huyo kufuatilia dokumenti zake ikiwamo bima na kumpeleka hospitali ya taifa kwa madai ya kuwa na ugonjwa wa akili jambo ambalo kijana huyo alikana na kusema walitumia mbinu chafu ili kukwepa kutoa ushahidi juu ya tukio.
"" Nimefanyiwa kitendo cha kinyama, unajua mimi wakati naitwa na walinzi sikufahamu naitiwa nini, wakati nafika waliniweka chini ya ulinzi na kuanza kunipiga wakanichukulia simu zangu pamoja na pesa shilingi laki 8, kisha wakanifunga pingu kwa nguvu na kunipakiza katika gari la zahanati yetu ya duce na kunipeleka hospitali ya temeke, cha kushangaza baada ya hapo ilitoka rufaa tena mara ya pili nihamishiwe muhimbili wakidi mimi naugua uchizi lakini hii yote ilikuwa ni mbinu za kunifanya nishindwe kutoa ushahidi, hivyo nilipokelewa kwa oda ya mahakama na kulazwa muhimbili kwa siku 20, lakini nilijaribu kukwepa vizingiti vyao vya kunihudumia kwakuwa sikuwa kama wanavyodhani, ila hakuna hata uongoiz wa chuo uliokuja hospitali mapaka natolewa""amesema Ccornel
amemuomba Mkurugenzi wa NHIFf kutokulipa gharama za matibabu kwani waliotakiwa kulipa ni uongozi wa DUCEe kwa kitendo cha kulaghai bima yake kwa kumtibu ugonjwa ambao hakuwa nao.
Hata hivyo, kwa kitendo alichofanyiwa amemuomba Waziri wa afya kuingilia kati sakata hilo kwani kitedno cha Madaktari kuruka mamlaka ya watu wengine ni kinyume na sheria hivyo kukomesha mara moja kwa wale wenye tabia kama alizozifanya daktari wa duce kumkatia rufaa mara mbili.
Ameenda mbali zaidi mara baada ya kuitaka na kuiombva Wizara ya Sheria na katiba kuwa macho na kuangalia kwa umakini utaratibu wa kuwalaza wagonjwa wenye ugonjwa wa akili katika hospitali kwa kufuata oda ya makama, kwani kitendo hicho kinaweza kukandamiza uhuru na kumnyima mtu haki yake ya kujielezea panapo hitajika ushahidi wa kina kama alivyofanyiwa yeye.
Licha ya kuomba PF3 3 ya mwanzo kushuhurikiwa ili waliomfanyia ukatili huo wakamatwe mara moja lakini alienda mbali zaidi akimuomba waziri mwenye dhamana ya elimu , mh ndarichako kuipa nguvu chama tcu ili iwe na kinga kubwa ya kuwatetea wanafunzi pindi wanapokutwa na majanga.
Amesma kuwa suala hilo watu wasiingiz e siasa wala kuwasingizia serikali, bali huo ni mpango mkakati uliopangwa na watu wachache wenye nia ovu na wasiopenda maendeleo , hivyo kwa serikali tulivu iliyopo madarakanai ana amini sheria zitafuatwa na wahusika wote watatiwa hatiani.
Smetoa shukrani kwa Uongozi wote wa Manispaa ya Temeke kwa kuwa naye bega kwa bega huku shukrani kubwa akimwagia afisa elimu shukle za msingi manispaa ya temekea kwa kuwa naye karibu kumliwaza pamoja na kumshauri mambo mengi ikiwamo kumtia moyo.
Aidha, ameiomba Serikali kuptia Vyuoni kukagua kuona ni kwananmna gani vyuo vinaendeshwa na kugundua watu wasiokuwa na malengo mazuri juu ya wanafunzi kwani ana amini kwamba kitendo alichofanyiwa siyo wa kwanza kufanyiwa wapo wengi wanafanyiwa semayea taarifa zao zinafichwa.
Naye mazzi wa kijana huyo, Gracious Mwanguya, amesema kitendo cha mwanaye kufanyiwa ukatili huo anakilaani kwa nguvu na amekiita ni unyanyasaji uliokithiri kwani tangia waanze kuwa na makuzi ya kijana wao hata siku moja hawajawahi kuletewa kesi hivyo ameushangaa uongozi wa duce kwa kutokuwa karibu na familia badaka yake waliamua kujifanyia mambo kienyeji bila ya kushirikisha famia yake.
Amesema kuwa kwa ssa wanasubiria kuona kesi hiyo ikiendeshwa na washtumiwa wakifikishwa katika vyombo vya sheria, kwani kitendo walichokifanya sio cha kiungwana katika maendeleo ya elimu hapa nchini.
""Huyu ni kijana wangu wa kumzaa, hajawahi kuwa na tabia mbovu, lakini mbaya zaidi niliposikia amepigwa na walizni, je ni sheria gani na eneo gani la kikatiba linasema mlinzi ana haki ya kumpiga mwanafunzi ? kwani hakuna sehemu ya kutatua matatizo mpaka wamfanyie unya huo? sasa sisi tunachoomba kwa serikali ni kupatiwa ufumbuzi wa suala hili katikia sehemmu husika nasi tujiridhishe kwa macho, leo tukiliachi hili la mwanangu kesho la mtu mwengine je ndiyo misingi ya sheria inatuelekeza tufanye hivi? tushaenda polisi na kila mahala tumetoa taarifa tunasubiria kusikilizwa""amesema Mzee Mwanguya
Amesema tukio la kijana huyo kupigwa lilitokea tarehe 3 ya mei mwaka 2018, baada ya kutokea tukio hilo waliripoti kilwa road kwa ajili ya kupatiwa PF3 na kupelekwa Temeke kabla ya tarehe 5 kufikishwa Muhimbili katika wodi ya wagonjwa wnaougua akili kwa kumfunga pingu.
Aidha, mzee mwanguya, ameomba Chombo chochote kinachojihusisha na saikolojia na ushauri kimsaidiae kiajana wake kwani kitendo cha kukaa wodi ya wagonjwa wasio na akili kimemfanya kidogo kuathirika japo sio sana.