bilioni 8.5 kujenga machinjio ya kisasa Vingunguti



Zaidi ya shilingi bilioni 8.5 zinatarajiwa kutumika kwenye ujenzi wa machinjio ya Vingunguti ili iweze kuzalisha nyama yenye ubora wa kimataifa na kuwaongezea tija wafanyabiashara.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Naibu Meya wa manispaa ya Ilala na Diwani wa kata ya Vingunguti (CUF)Omary Kumbilamoto kwenye kikao alichowakutanisha  wafanyabiashara wa machinjiona diwani huyo lengo ikiwa ni kuona jinsi ya kupata eneo mbadala la kufanyia biashara zao ndogo ndogo za nyama.
Aidha ameeleza kuwa anatambua umuhimu wa wafanyabiashara katika machinjio hiyo kwani biashara zao wanazofanya zimesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza matendo ya kihalifu katika maeneo hayo.
Amesema kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara hao diwani kwa kushirikiana na almashauri ya jiji pamoja na maafisa afya wanatarajia kwenda kutembelea eneo ambalo limepatikana kwa ajili ya wafanyabiashara pia kuona kma linakidhi mahitaji kwa mlaji
Kwa upande wake Afisa afya wa mazingira kwa niaba ya Afisa mtendaji wa kata ya Vingunguti Hamisa Mtendamema amewataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wakipata eneo lingine wanazingatia vigezo vya Afya vinavyotakiwa na TFDA ikiwemo usafi wa mazingira mavazi na vibali kwa ajili ya biashara zao.
Naye Mwenyekiti wa chama Cha wafanyabiashara Joel Meshack amewaomba wafanyabiashara kujijengea tabia ya kuishi kwa kufuata sheria na kanuni za kufanya biashara haswa kwenye suala la Afya na kuacha kufanya kazi kwa mazoea .
Machinjio ya Vingunguti ilisitisha kuuza nyama za kupima kwa kilo kuanzia Juni mosi mwaka huu kwa agizo la Mkurugenzi wa manispaa ya Ilala baada ya kuagizwa na mamlaka ya chakula na dawa TFDA ambapo kuanzia July mwaka huu ujenzi wa machinjio hiyo kwa kiwango Cha kimataifa utaanza.

Related

habari 4022159445048146671

Post a Comment

emo-but-icon

item