Wahanga wa Namaingo Agency waiomba Mahakama kumshikilia tena Mkurugenzi wa Taasisi hiyo


Image result for DC MJEMA AAGIZA MKURUGENZI WA NAMAINGO AGENCY KUKAMATWA


WANACHAMA,wa zamani wa Taasisi ya Namaingo Bussines Agency  ,wameiomba Serikali pamoja na Mahakama kuhakikisha wanamrudisha tena Mkurugenzi wa Namaingo Agency, mara baada ya kutoka kwa dhamana huku wakidai kwamba hawakutendewa haki kwa madai ya  kwamba kukaa kwake  nje kwa dhamana anaweza kuharibu  ushahidi wote.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mapema kwenye ofisi za utoaji wa a maelezo katika kitengo cha upelelezi cha makosa ya kifedha kilichopo chini ya Mkurugenzi wamakosa ya Jinai(DCI) kwa madai ya kutapeliwa na mkurugenzi wa kampuni hiyo,Biubwa Ibrahim zaidi ya Sh 1.5 bilioni.

Kiongozi wa Wahanga hao, Amosi misinde, amesema haki haikutendeka kwani tangia atoke kwa dhamana amekuwa akituma meseji kwa Wanachama wengine huku wengi wao wakiombwa kuandika maelezo  ile hali wao sio waliofungua kesi. 


Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa wilaya ya Ilala,Sophia Mjema kumuagiza Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala kumkamata na kumuweka ndani mkurugenzi huyo kwa kuwatapeli wanachama hao.

Kiongozi wa wahanga hao,Amosi Misinde amesema  Mei 4 mwaka huu walifungua kesi katika kituo cha polisi Msimbazi ambapo jarada lao lilipelekwa Kituo Kikuu cha Polisi na kuhamishiwa katika kitengo cha upelelezi cha makosa ya kifedha chini ya DCI.


"Mei 9 mwaka huu mkurugenzi wa kampuni hiyo alijisalimisha katika kituo cha polisi mkoa wa Ilala na siku hiyo hiyo aliletwa hapa kwenye kitengo cha upelelezi DCI na ofisi yake ilipekuliwa na kuchukuliwa kompyuta na baadhi ya nyaraka mbalimbali,"amesema Amosi 

Misinde alisema walishangazwa kuona siku alipokamatwa mkurugenzi huyo alitolewa kwa dhamana ambapo lile agizo la mkuu wa wilaya la kumuweka ndani  halikutekelezwa 

Amesema kuwa leo ni siku ya mwisho kuandika maelezo yao  kwa  DCI , hivyo jumla ya watu wengi wamejitokeza kuandika maelezo t , ambapo jumla ya Wanachama 150 wameshaandika maelezo kwenye Ofisi za DCI wengine wasio andika watafanya zoezi hilo baadae.

Amesema kuwa baada ya kuwa huru, mama huyo amekuwa na kazi ya kuwatumia wanachama meseji za kuwahamasiha , huku akiwaambia wawe na subira kwani watakutana ili kujadili maendeleo ya miradi yao.

Mmoja wa wahanga waliotapeliwa na Taasisi ya Namaingo, Regna Mutainurwa, alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuona wanapata haki zao, mara baada ya kuongea nae ameseman lengo ni kuona wanapata haki zao hivyo Mkuu wa Wilaya pamoja na vyombo husiaka wawasaidie  kwani wanateseka sana kutokana na fedha zao kuchukuliwa bila kuzifanyia kazi zozote na kwa maslahi ya mtu mmoja.

Mama huyo, amekuwa ni miongoni mwa wa mama waliojikita katika kuhakikisha waondokana na umasikini, ambaye alifika . katika ofisi za DCI,  alijiunga  na taasisi hiyo huku yeye akiwa mhamasishaji mkubwa  , lakini kubwa zaidi ni kuweka tawi lake kwenye ofisi yake ikiwa ni moja ya matawi yake mara baada ya mkurugenzi huyo kumuomba eneo kutokana na wingi wa wawatu na kupunguza adha za mizunguko ambayo ingekuwa gharama kubwa ya usafiri. mizunguko msongamano
Hata hivyo, mama huyo alifanikiwa kuongeza  Wananchama, kwani katika jitihada zake aliweza kufikisha jumla ya Wananchama 100 awali huku  wananchama 200 waliowapata ilitokana na jitihada za watu wengine waliotumka kama hamasa na wakala wa taasisi hiyo.

Aidha, mbali na kutumia nguvu nyingi kuhamasisha wenzake, lakini ofisi ya tawi hilo katika Wilaya ya Temeke ilikuwa katika nyumba yake mara baada ya kupangishkribani shilingi laki 8.

Amesema kuwa, baada ya kuona mama huyo amekuja na mipango na sera nzuri za kuwakonmboa na umasikini, aliamua kuchukua uamuzi wa kuingiza hadi familia yake na kujikuta akitumia shilingi milioni 1 na elfu 80 kama gharama zote alizotumia tangia ajiunge na taasisis hiyo.

Ameiomba Serikali kuingilia kati huku akimuomba Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia  Mjema, kuwasaidia kuapata haki zao kwani bado huyo mama tangia aachiwe kwa dhaman  amekuwa akiendelea kuwahamasiha watu kimya kimya akiwataka waendelee kuwa na subira ili azidi kuwaibia.

katika makubaliano maalumu na Mkurugenzin wa taasisi hiyo ila baada ya mambo kwenda kombo alijikuta akishindwa kupewa haki yake ya kodi iliyofikia tjpngine aao, mmoja wa wahanga waliotapeliwa na Taasisi ya Namaingo, ...... alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuona wanapata haki zao, mara baada ya kuongea nae ameseman lengo ni kuona wanapata haki zao hivyo mkuu wa wilaya pamoja na vyombo husiaka wawasaidie  kwani wanateseka sana kutokana na fedha zao kuchukuliwa bila kuzifanyia kazi zozote na kwa maslahi ya mtu mmoja.


Amesema kuwa mara baada ya kutoa Ofisi hiyo, walisajili jumla ya Wanachama 300, watu hao walitumika kama mawakala na wahamasishaji wa kampuni hiyo.

lakini anasema mbali na ofisi hiyo kuitoa makubaliano yao ya kimkataba walishindwana kutokana na kutolipwa kodi zake ambapo mpaka sasa anamdai jumla ya shilingi 800000, pamoja na pesa aliyotapeliwa baada ya kujiunga ni shilingi milioni moja na elfu 89.

Mwanachama Seledina Godfrey amesema aikiwa nyumbani kwake saa  saa10 jioni nilitumiwa meseji na mkurugenzi huyo kuwa niwe mvumilivu kwenye kipindi hiki kigumu hivyo viongozi tunaendelea kwabkaribu ili tuweze kuona jinsi gani ya kukutana tuweze kujadili maendeleo ya kampuni yetu.

Tukumbuke kwamba, Mkuu wa Wilaya ya Ilala,Sophia Mjema alimuagiza  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala amkamate na kumuweka ndani Mkurugenzi wa kampuni ya Namaingo Business Agency,Biubwa Ibrahim kwa madai ya kuwatapeli wanachama wake zaidi ya Sh1.5 bilioni.

Hayo yamekuja baada ya wanachama hao kumlalamikia mkuu wa wilaya hiyo wakidai kuwa mkurugenzi huyo amekuwa akiwachangisha fedha hizo akidai kuwa angewawezesha kiuchumi. Akizungumza na Digital Leo(Ijumaa)Mjema amsema mkurugenzi huyo aliitwa kwenye kikao kwa mkuu wa wilaya huyo alichokaa na wanachama hao kwa siku mbili ili wazungumzie suala hilo lakini hakutokea.


Mjema amesema mkurugenzi huyo aliwaahidi wanachama wake kuwfunguliwa miradi mbalimbali ambayo waliokuwa wakichangia kwa zaidi ya miaka mitatu lakini hadi leo hii hakuna alichowafanyia.

“Inanishangaza sana tangu mwaka 2016 huyu mkurugenzi amekuwa akiwaambia kila wanachama wake atoe fedha ili afunguliwe miradi ikiwemo wa Sungura,kununuliwa mashamba hekari tano,Mfuko wa bima ya Taifa NHIF na mizinga ya nyuki 50 lakini hadi leo hii hakuna kilichotendeka.
Namuagiza kamanda amkamate leo na kumuweka ndani na ofisi yake ifungwe isifanye kazi tena na afunguliwe mashtaka ili aweze kuwarudishia fedha wanachama wake,”amesema Mjema.
Mmoja wa wanachama hao,Renalda Mrema alisema alijiunga mwaka 2016 katika kampuni hiyo akiahidiwa atawezeshwa kiuchumi matokeo yake amepoteza zaidi ya Sh3 milioni alizokuwa alizochakia kwa kipindi cha miaka mitatu.

“Niliambiwa nitoe Sh250,000 kwa ajili ya kujiunga ,mkataba Sh20,000,bima ya afya NHIF Sh 76,000,usajili wa jina la biashara Sh45,000,kukaguliwa Sh20,000,darasa la hesabu Sh50,000,darasa la ufugaji wa samaki Sh50,000 na ufugaji wa nyuki 50,000.

Kila mwezi nilichangia mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo PSPF Sh10,000,NSSF 20,000,darasa la mafunzo ya SIDO Sh 50,000,darasa la ushawishi na utetezi Sh50,000, na darasa la mchakato wa masoko Sh50,000 lakini hakuna chochote tulichowezeshwa,”amesema Renalda.







Post a Comment

emo-but-icon

item