PRST kufanya kongamano la wiki ya mawasiliano Afrika
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/prst-kusherekea-kilele-cha-siku-ya.html

TAASISI ya Uhusiano wa Umma Tanzania, (PRST) , ipo mbioni kufanya kongamano kubwa la wiki ya Mawasiliano Afrika, ikiwa na lengo la kuona ni kwa jinsi gani taasisi hizo zinavyoweza kuchochea uchumi wa pamoja Barani Afrika ,ambapo Kitaifa inatarajiwa kufanyika kwenye Ofisi ndogo ya Bunge iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe25 Mei, mwaka 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Chuo cha Uandishi wa habari, SJMC,kilichopo Makumbusho Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Chama hicho hapa Tanzania, Ndege Makura, amesema ili kufanikisha siku hiyo wameamua kuweka mezani maada inayoendana na agenda kuu ya siku hiyo Kitataifa ya uchumi wa pamoja barani Afrika, wao wamekuja na tanzania ya viwanda.

Amesema kuwa ,kongamano hilo linafanyika kwa mara ya pili ambapo mara ya kwanza tanzania ilishindwa kuandaa kutokana na kukosa mwamko tofauti na sasa.

Hata hivyo, amesema kuwa katika kongamano hilo, yapo malengo bainishwa Kimataifa huku Bara la Afrika wakijadili uchumi wa pamoja lakini kwa Tanzania watajadili suala la mchango wa Maafisa Uhusiano wa Umma ni kwa jinsi gani wanaweza kuchangia kuleta maendeleo ya uchumi hususani katika suala zima la Tanzania ya viwanda.
"Hii ni siku muhimu kwetu watu wa Uhusiano wa Umma , kwani tutajadili vitu vingi vinavyotokana na Sera za maendeleo ya Taifa, wapo watu wengi hawaelewi nini maana ya Viwanda,dhumuni lake na njia za kufikia ndoto hiyo ya Rais wetu,hata Bungeni tumeona Wabunge wakikinzana kuhusu viwanda, tunaleta mjadala huu ili kujadili kwa kina na wataalamu wetu , Wizara ya Viwanda, Afisa uhusiano wa umma kutoka Serikalini na Taasisi binafsi, waandishi wa habari, ili kusaidia ndoto ya ya Rais kuimba wimbo wa pamoja wa Tanzania ya viwanda" amesema ndege
"Wapo baadhi ya watu hawatambui dhana ya Viwanda na maana yake hivyo wanajikuta kila mtu akiimba wimbo wake ,tunataka tuimbe wimbo mmoja, tumeshuhudia Rais wetu Magufuli,Mawaziri wetu na Wabunge wetu tukiwaachia waimbe wao wimbo huu haipendezi lazima wote tupaze Sauti kwa maendeleo ya Taifa letu"ameongeza Ndege.
Katika hatua nyingine,Rais wa PRST, Loth Makuza ,amesema kuwa wanakwenda kufanya tathimini yao katika kuchochea vugu vugu la maendeleo hapa nchini, kwani wamegundua asilimia kubwa ya kufikisha ujumbe kwa Jamii inatokana na wao hivyo watatumia kilele hicho kama njia ya kuona Sera za Maendeleo na wao wanashirikishwa .
Amesema kuwa changamoto nyingi za kutokukamilika kwa Sera mbali mbali za maendeleo hapa nchini kutofikia lengo ni kutokana na kutoshirikishwa hivyo watu wamekuwa wakichelewa kupata taarifa na kujua kwa kina juu ya utungwaji wa Sera hizo. ,
" Tunapo taka kufikia mafanikio yoyote Yale ushirikishwaji ni jambo la muhimu sana, hususani katika utungwaji wa Sera za maendeleo, Sera zetu nyingi zinatungwa katika lugha ngumu sana, hivyo tunaposhirikishwa inatubidi kuitafasiri lugha hiyo na kuwapa taarifa waandishi wa habari kuhabarisha Umma, kwahiyo zipo changamoto nyingi lakini hii ni lazima tukaijadili hiyo siku"amesema Lota.
Amesema katika kilele hicho cha siku ya mawasiliano ,wamepanga kuwashirikisha Waalimu wa Vyuo vinavyofundisha taaluma hiyo ili kujua njia gani , wanatumia kuwafundishia wanafunzi hao.
Amesema kuwa baada ya kilele hicho kila Nchi itatuma taarifa zake Makao makuu na baadae zitatumwa ripoti ya pamoja ili kubadilishana mawazo na Mataifa mengine kuona wao wanachukua hatua gani kuchangia uchumi wao katika taasisi hizo.
Amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi ili kuchangia mambo ya msingi yanayohusu maendeleo ya Taifa letu pamoja na uchumi wa pamoja katika Bara letu la Afrika.
Barani Afrika Makao Makuu ya Taasisi ya Uhusiano wa Umma yapo mjini Lagos Nigeria na duniani hapo uingerezaIkumbukwe kwamba , taasisi hiyo ilizinduliwa rasmi mwaka jana Novemba 2, mwaka 2017, Jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania, huku ikitimiza zaidi ya wanachama 200, ambapo miongoni mwao wametokea kwenye Taasisi binafsi walizo ajiriwa na wengine kutoka Vyuoni .
zoezi la kujiunga linaendelea kwa yule atakaye kidhi vigezo ambapo vigezo vilivyobainishwa mpaka sasa ni kuwa mfanyakazi wa kuajiriwa kwenye taaluma pamoja na mwanafunzi anayesomea hiyo taaluma.