Simba yakoga minoti ya Sportspesa leo

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/simba-yaanza-kukoga-manoti-ya-sports.html

KLABU ya soka ya Simba leo Alhamisi tarehe 24 Mei, Mwaka 2018 imekabidhiwa hundi ya Shilingi Milioni 100 na Kampuni ya Sportpesa lLmited ikiwa ni kutekeleza moja ya mkataba wao katika udhamini huo.

Hafla hiyo fupi ya makabidhiano imefanyika kwenye Ofisi za Sportspesa zilizopo Masaki Jijini dar es Salaam, huku tukishuhudia viongozi wa pande zote mbili sambamba na wachezaji na nahodha wao John Boko.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa Sportspesa, Tarimba Abbas , amewapongeza wachezaji wa Simba na viongozi wao kwa jitihada za kutwaa Ubingwa huo.
""Nichukue nafasi hii kuwapongeza viongozi na wachezaji wa Simba sc kwani mmewapa heshima kubwa wana Msimbazi nchini kote na kikubwa zaidi ni heshima mliyotupatia sisi wadhamini wenu wakuu , tunataka jitihada hizo mzipeleke kwenye kombe la Super cup sporstpesa nchini kenya ifikapo Juni 3 Mwaka huu""amesema Tarimba
Amesema kuwa Simba imeitendea haki nembo ya Sportspesa, huku akimamini kwamba wadhamini hao imekuwa moja ya chachu iliyopelekea simba kuchukua Ubingwa huo.
Tarimba amesema kuwa, walichokifanya leo ni kutimiza moja ya ahadi ambazo walizitoa wakati wa makubaliano ya kusaini mikataba mwezi Mei Mwaka jana kwamba watatoa bonasi ya shilingi miMilioni 100 kwa Timu yoyote ambayo imewadhamini na kuchukua ubingwa wa Ligi kuu , hivyo bila shaka Simba imelifanya hilo na wametekeleza kilicho walichokiahidi.
Akiongea kwa niaba ya Simba SC, Makamu wa Rais wa klabu ya simba ambao ni Mabingwa mara 19 wa Tanzania Bara , Salim Abdallah, ameishukuru kampuni ya Sportspesa kwa kuwa nao bega kwa bega
""Moja ya jambo ambalo klabu yetu imejivunia mwaka huu ni kuwa na wadhamini kama Sporstpesa ambaye mbali na udhamini wameweza kushirikiana na sisi katika shughuli mbali mbali ya uongozi , tulifanya maandalizi mazuri sana msimu huu kuanzia kwenye ngazi ya Uongozi hadi Benchi la Ufundi na ndio maana sio jambo la ajabu kuchukua Ubingwa kwani tuliweka mikakati na kushirikiana na wadhamini wetu wa Sportspesa, nawashukuru nawapongeza sana kwa moyo wao wa kuleta mabadiliko ya Soka hapa nchini ambayo sisi kama Simba tumeyaona kwa upande wetu na tutaendelea kutoa ushirikiano katika miaka mingine minne iliyosalia kwenye makataba wetu""amesema Kajuna
Naye Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameipongeza Sportpesa kwa kuharakisha kutoa fedha hiyo mapema hata kabla ya Ligi kumalizika.
Manara amesema kuwa kwa sasa kilichobaki mbele yao ni kombe la SportPesa (SportPesa Super Cup) litakalofanyika nchini Kenya na ameahidi kuwa mwaka huu ni lazima klabu yake itachukua kombe hilo na kwenda Mjini Liverpool, Uingereza kuvaana na klabu ya Everton.
Ikumbukwe kwamba,simba ni miongoni mwa Vilabu vinne kutoka Tanzania vitakavyoshiriki kwenye Michuano ya Sportspesa Super Cup inayotarajia kufanyika kuanzia Juni 3-10 ikishirikiana na timu nane kutoka Tanzania na Kenya.
Timu nyingine zitakazo shiriki michuano hiyo ni pamoja na Yanga, Singida united, na jku kutoka Tanzania samba mba na Gor Mahia, FC Leopards, Kakamega Home Boys sambamba na Kariobangi Sharks kutoka Kenya ambapo mbali na kujizolea kitita cha dola 30,000 , bingwa wa michuanao hiyo atapata nafasi ya kwenda Uingereza kucheza dhidi ya timu ya Everton FC kwenye Dimba la Goodison park.