Diwani Kumbilamoto atekeleza kwa vitendo agizo la Rais la Elimu bure
https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/diwani-kumbilamoto-atekeleza-kwa.html
DIWANI wa Kata ya Vingunguti ambaye pia ni Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto, leo amekabidhi jumla ya Mikeka 20 ya kukalia
Watoto katika Darasa la awali katika Shule ya Msingi Miembeni iliyopo Kata ya
Vingunguti Wilaya ya Ilala Jijini Dar es
Salaam ikiwa ni kuonyesha ni kwa jinsi gani anatekeleza agizo la Rais la elimu
bure.
Akizungumza na Raia Tanzania Online, Kumbilamoto
amesema kuwa msaada huo ni moja ya kuhakikisha Watoto hao wanaishi katika
mazingira mazuri ya kusomea ili kusaidia kuinua Elimu katika Kata yake akiamini
kwamba msingi mzuri wa Elimu unaanzia katika Elimu ya awali {chekechea).
Katika hafla fupi hiyo ya kukabidhi Mikeka, pia
amepata fursa mbali mbali ya kukutana na Wazazi wa watoto hao na kuwashukuru
sana Waalimuna Wazazi kwa umoja wao wanaouonyesha katika kukuza elimu za watoto
hao.
""Nipende kuchukua nafasi hii
kuwapongeza Waalimu wa shule hii kwa jitihada za kuwafundishi hawa hawa watoto,
maendeleo yoyote duniani yanatokana na elimu bora, hata tunaposema tanzania ya
viwanda lazima tutambue kwamba hatuwezi kuacha elimu nyuma, msingi wa elimu ni
elimu ya awali, hivyo nipende kuwaomba wazazi na waalimu shirikianeni kwa
pamoja kusongesha gurudumu hili la elimu mbele, kama wazazi mtakuwa pamoja na
waalimu tuna imani tutatengeneza kizai bora chenye manufaa kwa kata yetu na
taifa kwa ujumla, hiki ni kidogo nimebarikiwa nawaomba mkipokee tutazidi
kushirikiana kwa kila jambo"" amesema Kumbilamoto
Amewaomba Wazazi wa kata hiyo kuhakikisha kila
mtoto anasoma kwa vile Rais Magufuli ameleta elimu bure, hivyo hakuna sababu ya
mzazi kumuweka mtoto wake nyumbani wakati elimu ni bure ,
Hata hivyo amewatakia Waislamu wote waliopo
katika mfungo wa ramadhani, waingatie mafundisho yaliyotolewa katika kitabu cha
dini huku akiwataka kumcha mungu na kuomba mazuri katika kipindi hiki hususani
kumuombea yeye aweze kutimiza kile alichowaahidi wananchi wake.

