Meya Chaurembo akabidhi bendera kwa wawakilishi Tanzania katika mashindano ya Quruan Afrika



MEYA wa Manispaa ya  Temeke , Abdallah Chaurembo leo amekabidhi  bendera kwa wawakilishi wa mashindano makubwa ya 19 ya  kusoma na kuhifadhi Quruan tukufu  Barani ambapo jumla ya wawakiishi wawili watapambanishwa na nchi nyingine.

Akizungumza na waandishi wa habri leo kwenye hafla fupi ya kukabidhi bendera kwa wawakilishi , yaliyofanyika kwenye Shule ya Al Hikma iliyopo Muembe Yanga Wilaya ya Temeke Jijinini Dar es Salaam, amesema kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa amani na wao wapo bega kwa bega kuona kila kitu kinafanyika kwa wakati na Jeshi la ulinzi litafanya kazi zake kwa umakini mkiubwa.
Aidha ameupongeza Uongozi wote wa Taasisi hiyo ya Al Hikma, kwa kuandaa mashindano makubwa kama hayo Barani Afrika kwani ni moja ya kuitangaza Tanzania na kuonyesha wao ni bora katika marejeo ya hadishi za Mtume {S.A.W} kwenye kusoma Quruan.
Hata hivyo amefurahishwa na utaratibu uliotumika katika kuwapata wawakilishi hao huku akisema ni moja ya uadilifu mkubwa ulioleta uswa katika jamii na kuwapata watu sahihi wa kuwakilisha Taifa hili katika mashindano hayo.
""Kuna watu watashangazwa sana na kupewa Bendera Vijana hawa, wapo wengi walishazoea wanamichezo, wasanii ndio wanaopewa bendera kuipeperusha lakini leo nimeoana ni vema kuwapongeza Al Hikma kwani wametambua umuhimu wa Taifa lao na kuonyesha ni kwa jinsi gani Taasisi hiyo inatambua  na kuijali taiafa lake kwani ndio wakati mzuri wa kulitangaza Taifa lao kama wanavyofanya mataifa mengine kwakweli nawapongeza sana tunacho omba ni kwamba ushindi tuubakize hapa kwetu kwa maana tutakuwa tumetangaza Taifa kwa upana wake pamoja na kuwaonyesha kwamba tupo vizuri katika masuala ya dini hususani kufuata yale amabayo Mtume wetu alituachia na kutuasa kuyafanya""amesema Chaurembo 
Amewaomba wakazi wa Temeke pamoja na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi kushuhudia Watanzania wakipeperusha bendera kwani mashindano hayo hayana kiingilio , lakini pia amewaomba kwa waislamu wote wanaofunga katika mwezi huu mtukufu wa ramadhani wawe na utaratibu wa kusoma Quruan kama mtume alivyosema kwenye vitabu vya dini.
Katika hatua nyingine, Mismamizi wa mashindano hayo ambaye pia ni mkurugenzi wa Al Hikma foundation, Sheykh Nurdeen Kishk,amesema kuwa mashindano hayo ni ya 19 kufanyika katika nchi yetu ambapo kila mwaka yanfanyika inapofikia katika  mfungo wa ramadhani.
Pia amesema jumla ya nchi 19 zimejitokeza kushiriki katika mashindano hayo , ambapo katika mashindano hayo wapo waageni walioalikwa miongoni mwao wanatokea mataifa kama vile Uingereza, Uganda, Afrika ya kusini, Omani, kenya na Arabia ya kusini.

Amesema kuwa lengo kuu la kufanya mashindano hayo ni kumtukuyza Mwenyezi Mungu kwa kushusha kitabu bora kwa umma wa kiislamu na kuweka mafundisho yaliyo wazi juu ya dini ya Kisslamu na maisha kwa ujumla 
Hata hivyo amesema kuwa haikuwa kazi rahisi kuwapata wawakilishi hao, kwani walitumia Demekrasia pana ya kushirikisha Mikoa yote nchini Tanzania pamoja na Visiwa vya Zanzibar huku wakifanya mchujo wa aina tatu hatimaye  kuwapata washiriki hao ambao ni Shujaa Suleyman kutoka Morogoro na mshiriki wa pili ni Mbwana Dadi Abdallah kutoka Kaskazini Pemba.

Naye Rais wa Shirikisho la Wanadhuoni wa Kiislamu Tanzania, Shekh Suleyman Amrani Kilemile, amewaomba wadau wajitokeze kwa wingi katia kushirikiana kuhakikisha tukio hilo linakuwa la kihostoria hapa nchini.
Amesema kuhifadhi  Quruan ni kielelzo tosha cha kwamba Mtume alihifadhi Quruan ,lakini amesema kwamba Tanzania imevunja rekodo katika Bara la Afrika kwa kuanzisha mashindano hayo.
""Hii ni fahari kwa kila Mtanzania, tunakwenda kushindana na Mataifa mengine hata kama tutashindwa japo sio mategemeo yetu lakini tutaonyesha kwamba Tanzania tunamchango gani katika kukuza elimu ya dni hususani kusoma Quruan tukufu huku tukiamini watanzania wanapenda Quruan , hivyo tuna amini tutafanya mashindano yetu kwa amani na ulinzi tosha kwa vile Serikali wamekuwa bega kwa bega na sisi kuanzia mwanzo hadi mwisho mapaka unaona Waziri Mkuu kakubari kuja maana serikali inatambua tukio hili kubwa la kihistoria ""amesema Kilemile 

Ameipongeza Serikali ya tanzania kwa kuheshimu uhuru wa kuabudu na kulinda amani za watu wake, kwani bila amani wasingeweza kualika wageni pamoja na kufanya ibada.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukumbi na mapambo, Shekh Haruna Jumanne, ameishukuru Serikali kwa kuwahakikishia usalama wa kutoahsa, huku pongezi zake za dhati zikienda kwa Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATA) kwa kuwakubalia ombi lao la kuruhusu Magari yote yafanye kazi katika njia moja bila kujali njia yake ili kuwaleta wale watakao kwenda uwanja wa Taifa kushuhudia mashindano hayo.
""Tumejipanag sana, wale wote wanahofia usalama wao, wasiwe na shaka kwani watakuja na kuondoka salama, napenda kusema njooni msikilize kile Vijana wetu walichojiandaa nacho kwani Quruan ni nuru hivyo tunaomba Mwenyezi Mungu atuangazie na nuru hii ili Taifa letu liwe lenye baraka na maendeleo kwa kila Mtanzania""amesema Shekh Haruna 













Post a Comment

emo-but-icon

item