MEYA MWITA KULISAIDIA JESHI LA ZIMAMOTO KUTATUA CHANGAMOTO ZAO.


Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akiwa na madiwani wa halmashauri ya jiji hilo wakikagua miradi mbalimbali inayojengwa.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akizungumza na madiwani pamoja na  askari wa jeshi la Zimamoto, walipofanya ziara ofisini kwao  leo.
................................................................

Jiji la Dar es salaam pamoja na viongozi wa Menejiment ya jiji leo wamefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo katika jiji hilo.

Ziara hiyo ambayo imeongozwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Isaya Mwita imelenga kutizama na kukagua maeneo ambayo yamejengwa na jiji kwa lengo la kuwanufaisha wananchi wa jiji hilo

Akizungumza katika moja ya eneo ambalo wamelitembelea eneo la Drimp lilipo Karume halmashauri ya Manispaa ya Ilala,Mstahiki Meya Mwita amesema eneo hilo limetengenezwa kwa lengo la watu kupumzika lakini pia watoto watapata sehemu ya kucheza michezo mbalimbali.


Hata hivyo  viongozi hao wamefanya ziara Jeshi la Zimamoto na uokoaji la  jijini Dar es salaam kwa lengo la kuboresha maendeleo ya jeshi hilo ili kuweza kuondokana na changamoto walizonazo ambapo Mstahiki Meya Mwita amesema watahakikisha wanawasaidia jeshi hili kuondosha baadhi ya changamoto zao.

Related

habari 6614782517695907782

Post a Comment

emo-but-icon

item