Barabara ya Buguruni Mnyamani kupatiwa ufumbuzi.

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/barabara-ya-buguruni-mnyamani-kupatiwa.html

BARAZA la Madiwani la Manispaa ya Ilala limesema kuwa kilio cha wakazi wa maeneo ya Buguruni kuhusu barabara ya Buguruni kwa Mnyamani kinatarajia kupatiwa ufumbuzi wak wakati wowote kuanzia sasa.
Kauli hiyo ilitolewa Jijini Dar es salaam na Kaimu Meya wa Manispaa hiyo Jacob Messy wakati akijibu swali la Diwani wa Mnyamani Shukuru Dede, alipohoji kuhusu ucheleweshwaji wa ujenzi wa barabara hiyo.
Katika kikao hicho Manispaa iliwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Kamati ya fedha na Utawala kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Januari hadi Machi.
Alisema ujenzi wa barabara hiyo unatarajia kupata ufumbuzi wake hivi karibuni na kwamba Wakala wa Barabara TARURA ndio wenye mamlaka ya kusimamia barabara za halmashauri.
Kwa upande wake Kaimu Mhandisi wa Manispaa ya Ilala Justine Magoda amesema ujenzi wa barabara ya Buguruni Mnyamani unatarajia kuanza mwezi huu mara baada mvua za masika kumalizika.
Mhandisi Justine alisema shilingi bilioni 2.5 zinatarajia kutumika katika ujenzi wa Barabara ya Mnyamani na kwamba itajengwa na Kampuni ya BECCO.
“Barabara hii hadi ukamilika kwake itajengwa kwa muda wa miezi sita, tunaomba ushirikiano mara baada ya kuanza kwa ujenzi huu”amesema Justine.
Naye, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Utawala, Waziri Mwenyevale, alisema Kamati ya fedha na Utawala imesimamia utekelezaji wa shughuli mbali mbali za uendeshaji na usimamizi wa miradi ya maendeleo kupitia vikao vyake vya kanuni.
Waziri alisema katika kipindi cha miezi mitatu yaani kuanzia Januari hadi Machi, mwaka huu kamati ya fedha na Utawala imesimamia mapato na matumizi ya Halmashauri ya manispaa ambapo imekusanya jumla ya shilingi bilioni 10.4.
Waziri alisema fedha hizo sawa na asilimia 88 ya makisio ya sh, 11,793,447,388.50 bila kuweka ushurub