RC Makonda anena mazito katika hafla ya makubaliano ya kutia saini mikataba ya bara bara Tarura.


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amehudhuria katika hafla fupi ya kutia saini makubalaiano ya ya matenegenezo ya bara bara kati ya TARURA na Wakandarasi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Manispaa ya Ilala, Arnautogro leo Jijini  Dar es Salaam.

 Akizungumza na waandishi wa habari  mapema leo, RC Makonda, ameupongeza  Uongozi wa awamu ya Tano uliopo chini ya Mh: Rais Magufuli kwa kuja na mfumo wa kusuluhisha changamoto ya miundombinu hususani Bara bara.
Aidha, RC Makonda, amesema kuwa imani yake katika makubaliano hayo ya kimkataba dhidi ya Wakandarasi ni kuona miundombinu inaboreshwa hivyo TARURA wanawajibu wa kusimamia vyema mikataba hiyo kwa uadilifu mkubwa na umakini wa hali ya juu katika kuona Jiji la Dar es Salaam linakuwa bora kuliko Majiji yote hapa Nchini.


Amesema kuwa Miongoni mwa majukumu makubwa ambayo TARURA wanatakiwa kufanya ni kutoa mwanga na kutimiza ndoto za Rais Magufuli za kutatua changamoto za kuboresha miundombinu hususani ara bara bora zitakazotumika katika kukuza uchumi wa Taifa letu.
Aidha, RC Makonda, amesema kuwa imani yake katika makubaliano hayo ya kimkataba dhidi ya Wakandarasi ni kuona miundombinu inaboreshwa hivyo TARURA wanawajibu wa kusimamia vyema mikataba hiyo kwa uadilifu mkubwa na umakini wa hali ya juu katika kuona Jiji la Dar es Salaam linakuwa bora kuliko Majiji yote hapa Nchini.

“”Napenda kuchukua nafasi hii kuwatahadharisha kwamba, kama kama wapo Viongozi  wa TARURA watajitokeza na kuendekeza rushwa na kuwaangusha Watanzania pamoja na ndoto za Mh: Rais Magufuli sitokubaliana suala hili, hivyo ikitokea nikajua nitawaajibisha kwa  mujibu wa sheria, hivyo niwaombe Viongozi wa TARURA, mjiepushe na  viashiria vya rushwa katika kumpata Mkandarasi na mtu wa tenda ili wafanye kazi vizuri katika ufanisi na utendaji wa hali ya juu”Amesema RC Makonda .

Hata hivyo, amewataka wale wote Wakandarasi waliosimamishwa katika utendaji mbovu wa bara bara , wahakikishe wanatafutwa na kuzijenga upya kwa gharama zao wenyewe.
Katika hatua nyingine,  RC Makonda amewataka TARURA wawe na utaratibu kuwasiliana na kushirikiana kwa ukaribu sana na baadhi ya taasisi kama vile Tanesco, Dawasco, pamoja na TTCL ili kuepusha gharama zisizo za kilazima wakati wa ujenzi wa bara bara na kurahisisha kukamilika kwa miradi mapema.
Pia, amewaomba TARURA, wawe na utaratibu wa kuwalipa mapema wafanyakazi wao pamoja na wakandarasi ili waendane na kasi ya utendaji , hivyo katika kufanikisha hilo amesema atakuwa na utaratibu wa kufanya ziara za kutembelea bara bara ambazo zimekabidhiwa kwa wakandarasi.
Ametoa wito kwa Wakandarasi wote walinde heshima za Kampuni zao ili wazidi kujijengea uaminifu na Serikali na kupatiwa tenda zaidi na kama kuna mtu atakwenda kinyume na kutothamini kodi za masikini na walala hoi hatosita kumshughulikia.
Amesema Mkoa wa Dar es Salaam ni mkoa wenye mabonde na miinuko mingi , hivyo kazi iliyokuwepo kwa sasa ni kuhakikisha kwamba  inabuniwa mipango bora  wa Mtaro ili ifikishe maji sehemu husika.
Ametoa wito kwa Waandishi wa habari, kuhabarisha Umma kwamba kila mwananchi atakaye taka kununua kiwanja ahakikishe anapata taarifa za kina juu ya eneo hilo ili asijekuingia kwenye migogoro.
Naye Katibu wa Bodi ya Zabuni wa Bara bara Mkoa wa Dar es Salaam, Devotha Ndusilo, amesema jumla ya miradi inayotarajiwa kufanywa na Wakandarasi hao itagharimu kiasi cha pesa taslimu shilingi Bilioni 5 na Milioni 86 laki 9 kwa ajili ya matengenezo ya Bara bara kiwango cha lami zenye Km 4.7, ambapo ujenzi huo utahusisha Box Culvets, bara bara za changarawe, na uzibaji wa viraka vya lami (patch works) kwenye bara bara ya Haile Selaise, Magomeni Makuti pamoja na Mwananyamala Kisiwani.
Hata hivyo, Mratibu wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam, George Tarimo, amewapongeza Wakandarasi kwa kupata tenda hiyo na kuwataka wafanye kazi kwa kuzingatia viwango na ubora kwa kuwa wanafungu la kutosha la kuhakikisha bara bara zinakuwa katika ubora wa juu utakao kidhin haja za watumiaji na kuchangia pato la Taifa.  

Related

habari 1748985160465638619

Post a Comment

emo-but-icon

item