Filamu iliyopigwa marufuku Kenya kuonyeshwa katika tamasha la filamu Cannes

Amber VallettaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanamitindo Amber Valletta, na simu yake ya mkononi ,kwenye tamasha ya Cannes
Tamasha la kimataifa la Cannes linaanza hii leo, siku moja mapema kama ilivyokawaida, na sheria mpya pia zimebuniwa kuhakikisha kila kitu kinaendela shwari kama kawaida.
Wageni wanaojipiga picha za 'selfie' kwenye zulia jekundu wanazuiliwa kama njia ya kukomesha tamaduni hiyo iliyokuwepo hapo awali.
Upeperushaji wa tamasha hilo kwa mara ya kwanza na vyombo vya habari kwa ulimwengu mzima hautafanyika tena kama ilivyokuwa awali.
Tamasha hiyo itashirikiana na serikali ya Ufaransa kubuni nambari za usaidizi kwa wanawake kuweza kuripoti visa vya unyanyasaji wa kingono.
Hii ni baada ya madai ya mzalishaji wa filamu Harvey Weinstein kumbaka muigizaji na kukosa maadili mema wakati wote anapohudhuria tamasha hizo.
Weinstein amepinga madai yote ya kufanya mapenzi bila idhini.
Maudhui ya filamu hiyo yanahusu mapenzi ya jinsia mojaHaki miliki ya pichaRAFIKI
Image captionMaudhui ya filamu hiyo yanahusu mapenzi ya jinsia moja

Mvutano kwenye sekta ya filamu

Filamu ya Kenya Rafiki, iliyopigwa marufuku nchini humo itaonyeshwa kwenye tamasha hilo nchini Ufaransa siku ya jumatano.
Hii ni mara ya kwanza kwa filamu yoyote kutoka Kenya kupeperushwa katika tamasha la Canne, lakini nchini Kenya filamu hiyo imepigwa marufuku kwa maudhui ya filamu yenyewe inayotajwa kushinikiza mapenzi ya jinsia moja.
Filamu hiyo inayoitwa 'Rafiki', inasimulia hadithi ya wanadada wawili ambao wazazi wao ni washindani wa kisiasa, huku wanadada wenyewe wakisalia wamependana.
Lakini mkurugenzi wa bodi inayodhibiti filamu nchini Kenya Ezekiel Mutua, alishutumu filamu hiyo akisema inajaribu kuonyesha kuwa mapenzi ya jinsia moja ni jambo la kawaida.
Alitaka mtayarishi wa filamu hiyo Wanuri Kahiu kuondoa sehemu ambazo alisema zinasafihi, pamoja na sehemu ambapo yamkini wadada hao wanafanya mapenzi. Lakini sehemu hizo hazikutolewa na filamu hiyo sasa hairuhusiwi kuonyeshwa nchini Kenya.
Bi Kahiu alisema kuwa amesikitika Filamu hiyo haitaonyeshwa nchini Kenya, akisema watu wazima ana uwezo wa kujiamulia maswala. Hata hivyo katika mahojiano yake mengi anapuuza swala la marufuku hayo, na badala yake anasisitiza tu umuhimu wa kunyeshwa kwa filamu hiyo katika tamasha za kifahari za Canne.
Mapenzi ya jinsia moja ni hatia nchini Kenya, na wanaopatikana na hatia wanakabiliwa na kifungo cha miaka kumi na nne gerezani.
Vuguvugu za kutetea haki za kundi hili pamoja na mataifa mengi ya kigeni yamejaribu kuishurutisha nchini hii kubadilisha sharia zake, lakini Rais Uhuru Kenyatta alisema hivi majuzi kuwa swala la haki ya wapenzi wa jinsia moja si jambo la kupewa kipau mbele machoni mwa wakenya.
Tamasha la mwaka huu ni la kwanza kufanyika tangu sekta ya burundani kugubikwa na visa vya unyanyasaji wa ngono.
Miongoni mwa bodi ya tamasha hilo ni muigizaji wa Ufaransa Lea Seydoux ,mmoja wa wanaomlaumu Weinstein kwa kutumia njia zisizo mwafwaka kwake.
Bodi hiyo itaongozwa na mshindi wa Tuzo za Oscars wa Australia Cate Blanchett na Kristen Stewart na nyota wa filamu za Twilight.
Nyota hao watatu wamefanya kazi na Woody Allen , ambaye analaumiwa na mtoto wake wa kambo Dylan Farrow kwa kumnyanyasa kijinsia kama mtoto.
Idadi ya waigizaji maarufu wamejitenga na muelekezi huyo ambaye amepinga mara kadhaa madai ya unyanyasaji.
Filamu ya Kitanzania kupaa anga za kimataifa

Waelekezi wanawake ndio walio wachache

Wanawake wamezidi idadi ya wanaume kwenye bodi ya mwaka huu, inayowajumuisha muelekezi wa filamu Ava DuVernay na mtunzi wa nyimbo wa Burundi Khadja Nin.
Bodi hiyo ya waamuzi inakamilishwa na muigizaji wa China Chang Chen na wanaume watatu waelekezi - Mfaransa Robert Guediguian, raia wa Canada Denis Villeneuve na Mrusi Andrey Zvyagintsev.
Katika orodha ya shindano hilo , wanawake ni wachache mno . Kati ya filamu 21 ni filamu tatu ambazo zinawaelekezi wanawake - kama ilivyokuwa mwaka jana.
Mfaransa Eva Husson , raia wa Lebanon Nadine Labaki na Mtaliano Alice Rohrwacher - ni hao pekee ndio wamekuwa kwa mashindaano yaliyopita.
Spike Lee, Jean-Luc Godard na Pawel Pawlikowski ni miongoni mwa waelekezi wanaume wanaoshindania kwa tuzo kubwa ya Palme d'Or.
Wanaungana na watu wengine ambao majina yao si maarufu kwenye orodha iliyoorodheshwa inayotajwa kama 'mshangao mpya' kwa viwango vya Cannes.
Jean-Luc Godard, Spike Lee and Pawel PawlikowskiHaki miliki ya pichaEPA/GETTY IMAGES
Image captionkushoto kuelekea kulia : Jean-Luc Godard, Spike Lee and Pawel Pawlikowski
Filamu nyengine ambazo zinawania tuzo kubwa kama ile ya Three Faces , ambayo iliongozwa na raia wa Iran , Jafar Panahi , amepigwa marufuku kuondoka nchini mwake.
Viongozi wa Ufaransa wameiomba serikali ya Iran kulengeza upigaji marufuku wa usafiri na kumruhusu Panahi kuhudhuria tamasha hiyo.
Pia hakuna uhakika iwapo muelekezi wa Urusi Kirill Serebrennikov, ambaye filamu yake ya Leto ambayo iko kwenye shindano hilo atakuwepo.
Muelekezi huyo wa filamu mwaka ujao alitumikia kifungo cha nyumbani baada ya kupatikana na hatia ya udanganyifu wa kifedha.
Na pia filamu ya The House That Jack Built, kuhusu mauaji ya kikatili (Matt Dillon) pia inarudi kwenye shindano hilo.
Muelekezi huyo raia wa Uholanzi alipigwa marufuku kutoka Cannes mwaka 2011 baada ya kudai kuelewa na kumuonea huruma Adolf Hitler katika muungano wa wanahabari.
Lars Von Trier na Kirsten Dunst
Image captionLars Von Trier na Kirsten Dunst
Mwaka uliopita Von Trier alikana kumnyanyasa Bjork baada ya mwanamuziki wa Iceland kumlaumu muelekezi ambaye hakumtaja kwa jina kwa kuonyesha tabia zisizofaa.
Von Trier amekuwa muelekezi wa filamu za Bjork hadi hivi sasa - 2000 ya Dance in the Dark.
Tamasha ya mwaka huu itafunguliwa kwa filamu ya Everybody Knows , filamu ya kusisimua inayowajumuisha wanandoa waigizaji Javier Bardem na Penelope Cruz.
Tamasha hiyo itakamilika wiki ijayo na filamu ya The Man Who Killed Don Quixote.Muelekezi wa filamu Terry Gilliam kila mara kuihairisha kuzungumzia filamu ya Miguel de Cervantes.

Related

KIMATAIFA 4952770166996976762

Post a Comment

emo-but-icon

item