Kumbilamoto awasaidia vikundi mbalimbali vya Wanawake na vya Michezo Vingunguti


Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vingunguti, Omary Kumbilamoto ametoa msaada wa fedha na vitu mbalimbali kwa vikundi mbalimbali vya wananchi wa kata ya Vingunguti kwaajili ya kujikwamua kiuchumi na kukuza maendeleo ya kata hiyo.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi msaada huo Kumbilamoto amesema  kuwa amewapatia msaada huo wananchi hao baada ya kuwasilisha kilio Chao kuwa wanayo mahitaji ya vitu vidovidogo kama mzani wa kupimia Mchele, chupa za kuzuia kahawa, kuongeza mtaji wa chapati, maandazi, na vitafunwambalimbali.

Vikundi vilivyonufaika na msaada huo ni JipeMoyo Vikoba,Nyota Njema kilichopo mtaa wa Majengo na Mzee Suleiman Chuma ambaye ni Muuza kahawa.

Kwa upande wao wanamichezo pamoja na wananchi walionufaika na msaada huo wameshukuru Diwani huyo kwa kuguswa na matatizo ya wananchi na kujitolea kuwasaidia kama alivyo ahidi kuwatumikia na kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali katika kata hiyo

Related

habari 2369531137337436245

Post a Comment

emo-but-icon

item