RC Makonda afurahishwa na kasi ya Ujenzi wa Ofisi za Waalimu






MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh: Paul Makonda amevutiwa na kasi ya ujenzi wa Ofisi za Waalimu katika mkoa wake mara baada ya kufanya ziara mapema leo na Waandishi wa habari katika shule ya Sekondari Kasulu iliyopo Wilaya ya Ilala na Shule ya Sekondari ya Makumbusho iliyopo Wilaya ya Kinondoni  ili kuona maendeleo ya miradi hiyo inavyokwenda lengo likiwa kila mwalimu ndani ya mkoa wake kuishi mazingira bora na kupata moyo wa kufundisha wanafunzi.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo mara baada ya kumaliza ukaguzi wa pili wa Ofisi za Waalimu uliopo katika Shule ya Sekondari Makumbusho iliyopo Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, RC Makonda amewapongeza kamati ya  Ujenzi kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kujitolea bila malipo huku akisema ni moja ya kuhakikisha maendeleo ya Elimu katika mkoa wa Dar es Salaam yanakuwa kwa kasi na kuongeza viwango vya ufaulu kwa Wanafunzi.
Aidha, amesema lengo la kujenga Ofisi hizo zenye jumla ya  idadi  402, ambapo jumla ya Ofisi 255 upande wa Shule za Msingi na 247 kwa upande wa Shule za Sekondari ili kuongeza kasi ya ufundishaji na kuwajengea mazingira bora ya kufundishia kwa Waalimu katika kuchochea maendeleo ya Elimu kama kauli ya Rais Magufuli ya Elimu bure inakamilika kwa vitendo.
RC Makonda amesema ndoto na shauku yake ni kuona Elimu Bora inatolewa ili kusaidia Taifa kuwa na Wataalamu wa kutoshakuepuka kuchukuwa Wataalamu kutoka Nje ya Nchina ili kufikia huko ni lazima Walimu wawekewe Mazingira Bora ya kufanya kazi kwakuwa tayari Rais Magufuli ameshaonyesha Dira kwa kutoa Elimu Bure ili kumwezesha Mtoto wa Maskini kuwa na utajiri na kunufaika na rasilimali za Nchi hii. 


""Ujenzi huu wa Ofisi hizi ni jitihada zangu kwa kushirikiana na wadau mbali mbali waliojitokeza kunisaidia ili kuboresha Mazingira ya Walimu , hili nililigundua baada ya kikao na Wakuu wa Shule na kugundua walimu wanafanya kazi katika Mazingira Magumu ikiwemo kufanya kazi zao Chini ya Miti na ukosefu wa Vyoo,  ""amesema RC Makonda .



RC Makonda amesema katika awamu ya kwanza watakabidhi  jumla ya Ofisi 150 na kuwaomba Wananchi kushirikiana na Serikali kwa kuendelea kuchangia kampeni hiyo ili kuwawezesha Walimu kufanya kazi katika mazingira mazuri.
Hata hivyo, RC Makonda amewataka Waalimu wafanye kazi kwa bidii na ujasiri mkubwa ili kutengeneza Taifa lenye ubora wa elimu katika kukuza uchumi wa Tanzania ya Viwanda, na kuwaomba Wanafunzi wajitambue na kuachana na mambo ambayo hayana maslahi nayo ya kipuuzi yenye lengo la kuwatoa kwenye njia ya elimu badala yake wajikite kwenye kusoma kwani elimu ndio msingi wamaendelo katika Taifa lolote linalokuwa kiuchumi.

Katika hatua nyngine, RC Makonda, amesema yapo mambo makubwa mawili ambayo mwaka huu anatarajia kuyafanya, moja ni kushindanisha kielimu  Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Mkoa wa Arusha kwani tayari washafanya mazungumzo na RCwrusha Mh: Mrisho Gambo ili kutanua wigo wa elimu hapa nchini na kuhakikisha kiwango cha ufaulu Mkoa wa Dar kinakuwa kwa kasi na washindi watapatiwa zawadi na wale Waalimu ambao masomo yao yatafanya vizuri watapatiwa fedha taslimu Milioni 10  pamoja na kuchagua Mbuga ya Wanya yeye na familia yake ili kutangaza utalii wa ndani.
""Nataka miaka 3 ijayo , shule za Mkoa wa Dar zishike nafasi ya 1 hadi ya 10, mkifanya hivyo nami nitafarijika sana na zawadi nitakazo wapatia hamtanisahau katika maisha yenu yote, niwaombe waalimu zingatieni maadli ya kazi zenu, wafundisheni hawa, ofisi zitakuwa nzuri, za kimataifa, shida yangu kubwa ni kuona tunapata matokeo makubwa katika Mkoa wetu""ameongeza RCMakonda.
RC Makonda amesema , wapo wadau wengi ambao wamejitokeza kuwasaidia wale wanaobeza maendeleo hayo waendelee kubeza wao wanasonga mbele,hivyo baada ya mwezi wa Ramadhani kumalizika ujenzi huo utakwenda kwa kasi kubwa. 

Post a Comment

emo-but-icon

item