Wakandarsi waitika wito wa RC Makonda kusaidia kuboresha miundombinu Dar

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/05/wakandarsi-waitika-wito-wa-rc-makonda.html
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam. Mh: Paul Makonda, leo amekutana na Wakandarasi wanaomiliki Kampuni kwenye Ofisi yake baada ya Wakandarasi hao kukubali wito wa kuwaomba kusaidia ukarabati na ujenzi wa bara bara zenye shida ambazo hazipo kwenye bajeti ya Serikali kuu ili kuwaondolea kero

Katika ombi lake dhidi ya Wakandarasi, jumla ya Kampuni 70 zimejitokeza kusaidia uboreshaji wa miundombinu , hivyo ni jukumu lao kuchagua maeneo ambayo wataona wana uwezo nayo kuyajenga na watafuata maelekezo kutoka kwa TARURA.
Akizungumza na Waandishi wa habari leo Ofisini kwake, amesema mpaka sasa wana waratibu watatu wanaohusika katika vyanzo mbali mbali vya mapato katika ujenzi wa miundombinu , miongoni mwa vyanzo hivyo ni pamoja na DMDP, TARURA pamoja na TANROADS.
RC Makonda amesema kuwa, miongoni mwa changanoto zinazoikabili bara bara za Mkoa wa Dar, ni kujenga bara bara bila ya kuweka mifereji ambayo inaelekeza maji kwenda hivyo kama zipo bara bara hizo basi Wenyeviti wa Serikali za Mitaa wahakikishe wanaziorodhesha bara bara zote zenye shida na kuwapelekea Meneja husika katika Wilaya yake ili ziweze kupatiwa ufumbuzi katika kuondoa kero zilizopo mtaani.
"'Nataka kuwaambia ndugu zangu, tunachangamoto kubwa sana kwenye mitaa yetu hususani suala la bara bara, nyumba nyingine zimezingirwa na maji, mitaro hakuna bara bara mbovu, hizi zote changamoto, nimeona nitafute wadau wanisaidie nashukuru mungu wamekubali kilichobakia ni utekelezaji, hivyo nawaomba na wengine wenye nia ya kutaka kutusaidia nawakaribisha, tukiwa na bara bara mbovu magari yana haribika, ajali zinatokea , hivyo tukishirikiana Tunaweza kutatua changamoto hizi kwa haraka na hatimaye tukawa na miuondombinu bora yenye kuvutia na kupelekea kukua kwa uchumi wetu ""amesema RC Makonda
Lakini amesisitiza kwamba mbali na kusaidiwa, Wenyeviti hao wawe na utaratibu wa kuchangia kiasi kidogo cha fedha ili kufanikisha zoezi hilo kwa ufanisi.
Amesema kuwa , kadri Wananchi wanavyozidi kulipa kodi , ndivyo kasi ya utengenezaji wa bara bara inakuwa kwa kasi kwahiyo ipo haja ya kila mtu kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa lake.
Amewataka wale watakao kuwa na shauku ya kutengeneza bara bara katika maeneo yao, basi wawasiliane na Meneja wa TARURA ili bara bara zao ziratibiwe na kujengwa kwa gharama nafuu itakayokizi matakwa ya kipato cha wachangiaji na shauku yake ni kuona mifereji yote yenye shida inatibiwa na kuleta muonekanao mpya .