Rais ametupa heshima wamachinga

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/02/rais-ametupa-heshima-wamachinga.html
MJUMBE wa Shina la Nyamwezi na Uhuru kupitia tiketi
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kariakoo, Abdarahaman Kaisi, ambaye pia
ni mfanya biashara ndogo ndogo maarufu kama mmachinga wa Kariakoo amemshukuuru
Rais Magufuli kwa kuwajali wamachanginga.
Hayo ameyasema baada ya kuwapongeza viongozi na
waasisi wa Chama cha Mapinduzi CCM, kwa kutimiza miaka 41 huku shukrani zake za
dhati zikimwendea hayati Mwalimu Nyerere kwa kukiongoza vyema chama tawala.
Akizungumza na Raia Tanzania, Kaisi, amesema ni
wakati sasa wa Wamachinga kutembea kifua mbele baada ya kumpata mtetezi wa
maslahi yao.
Amesema ni muda mrefu sana wamachinga walikuwa wakinyanyasika
lakini kupitia Rais wa awamu ya tano Mh:John Magufuli, amewaheshimu sana na kuwakumbuka baada ya kuwafanya
kufanya kazi zao kwa uhuru.
“Huyu ni Rais anayetujali, hakika wamachinga
tunajivunia, kinachotakiwa ni kupambana kufanya kazi kwa bidii na kulinda
sheria za nchi pamoja na kulipa kodi”,amesema Kaisi
Hata hivyo, amesmshukuru Mkuu wa Wilaya ya Ilala,
Sophia Mjema, kwa jitihada zake za kuhakikisha wamachinga wanakuwa na utaratibu
maalumu na wanafanya kazi kwa uhuru.
Mfanya biashara huyu wa kariakoo, amewataka wananchi
wajitokeze kuwaunga mkono kwani baiashara kwa sasa imekuwa ngumu kutokana na
hali ya uchumi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online