IYF yazindua mpango wa kumkomboa Kijana wa Kitanzania

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/02/iyf-yazindua-mpango-wa-kumkomboa-kijana.html
TAASISI isiyo ya Kiserikali kutoka nchini Korea
Kusini inayojishughulisha na masuala ya kuwajengea fikra na kuwasaidia Vijana
kutoka Mataifa mbali mbali hapa nchini (IYF) , leo wamezindua programu ya Vijana
ijulikanayo kama ‘Najivunia Tanzania kwa kazi za kujitolea Ng’ambo .
Uzinduzi huo umefanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah ulipo
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo ulihuzuliwa na Vijana kutoka sehemu mbali
mbali ikiwamo wanafunzi wa chuo hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi
mtendaji wa IYF kutoka Makao Makuu
nchini Korea Kusini, Prof: Seong Hum Kim, amesema lengo la mpangu huo ni kutaka
kuona Vijana wa Kitanzania wakitumia fursa mbali mbali ili kuleta maendeleo ya
nchi.
Amesema kuwa, Tanzania ni miongoni mwa Mataifa ambayo
yanawezza kuongoza Bara la Afrika kwa
kuwa na Vijana wenye ualedi mkubwa juu ya mitizamo kuleta maendeleo na kufanya
nchi hiyo kuwa moja ya Taifa lenye uongozi bora Afrika nzima.
Aidha, amesema kwa sasa Tanzania inakabiriwa na changamoto
ya ajira hivyo kuzindua mpango huo wa kutembelea nchi mbali mbali kwa kazi za
kujitolea utakuwa ni moja ya fursa kwa Vijana hao na kujitangaza Kimataifa
kutokana na shughuli wanazo zifanya.
“Tunaipenda Tanzania, ni moja ya Mataifa ambayo
uchumi wake unakuwa kwa kasi tumeona ili
kusaidia soko la ajira ni vyema tukawa bega kwa bega vijana hawa ili kufikia
malengo yao na kukuza uchumi wa Taifa mbali na hayo tutapata Viongozi bora
watakaoongoza kwa kufuata misingi ya sheria na kanuni huku roho kubwa
ikiwaongoza katika utendaji wao ni kuwa na hali ya kiuzalendo”, amesema Kim
Naye Mkuu wa program kutoka IYF hapa nchini, Prof:
Jeong Hee Yong, amewataka Vijana kuangalia fursa na kuachana na dhana ya
kuajiriwa kwani ajira zilizopo ni chache hazikidhi mahitaji ya Vijana wa
Kitanzania wote, hivyo kama watabadili fikra na kuangalia upande wa pili
anaimani watafanikiwa na kupelekea Taifa kuwa na uchumi imara kutokana na kuwa
na wataalamu mbali mbali watakao saidia kukuza sekta za uchumi hapa nchini
baada ya kupata maarifa kutoka nchi za nje.
Pia amesema mpaka sasa ni jumla ya Mataifa 80
yameomba watu wa kujitolea huku mpango wao kwa sasa ukiwa umefikisha jumla ya
Mataifa 25 ambayo shughuli za taasisi hiyo zimekuwa zikifanyika ikiwamo
Tanzania.
“Mwaka huu tunatarajia kuwa na Vijana 100 watao
jitolea, tunachosubiria kwa sasa ni ratiba zetu na ni wapi Vijana watapangiwa
ila idadi ya Vijana itaongezeka kadri ya mahitaji ”, amesema Yong
Hata hvyo kwa upande wa Afisa mahusinao ya Umma wa
IYF, Mwazani Ramadhani aliyesafiri nchi mbali mbali ikiwamo Korea Kusini ,
amekiri kuwepo na fursa nyingi kwa Vijana watakao bahatika kujiunga na shirika
hilo huku akiwataka Vijana wajitokeze kwa wingi kwani changamoto ya ajira
Tanzania ni kubwa , hivyo kwa kufanya kazi za kujitole kutawasaidia kujenge
mahusiano bora na Mataifa mengine.
“Tunaomba Vijana wajitolee, kuna Vijana wamejenga
dhana ya kwamba kujitolea ni kupoteza muda jambo ambalo kwa IYF sio kweli bali
utaweza kubadilisha fikra zako na kuwa na mtazamo chanya wa maisha”, amesema
Mwazani
Kwa upande wa Mshauri wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam , Paulina Mabuga, amewataka Vijana wanyanyuke na wachukulie fursa
hiyo kama ni ajira kwao kwa kufanya hivyo kutwaunganisha na Mataifa mbali mbali
katika kujenga umoja na kutafuta fursa za ajira.
Amesema wameanzisha Klabu ya IYF chuoni hapo, na
wanatarajia kuona matunda baada ya wanafunzi kujitolea kwani moja ya sifa itapelekea
kumjengea uwezo uwezo mwanafunzi wa kupambana na mazingira
tofauti inapofika suala la ajira.
“Hii ni njia bora kinachotakiwa ni Vijana kupambana,
wenzetu nafasi kama hizi zinawajengea CV, hivyo tunatakiwa tukizipata tuzitumie
kushiriki kikamilifu pengine tunaweza kushuhudia siku moja wimbi la ajira hapa
nchini likapungua kwa kasi na tukapata viongozi imara na bora”,amesema Mabuga
Ameupongeza Uongozi mzima wa IYF kwa kutambua
umuhimu wa chuo chao na kufanya semina hapo kwani wanajua fikra Mlimani ni Chuo
kikubwa ambacho kina beba zaidi ya maelefu ya wanafunzi ambao watakuwa mabalozi
wa kusambaza ujumbe kwa wenzao kuhusiana na kazi za kujitoea.
Miongoni mwa shughuli zinazofanya na taasisi hiyo ambayo
ina mipaka ya umri wa kujiunga kutoka miaka 18 hadi 35 ni pamoja na kusambaza
tamaduni kutoka Mataifa mbali mbali, kukuza maendeleo ya rasilimali za nchi na
kuziheshimu, kukuza uelewa na kubadilishana mawazo na mataifa mengine,
kuhamasiha soko la ajira na kuhakikisha mtu anafurahia kujitolea kwa ajili ya
kujenga mawazo mapya kwa maisha yake ya baadae.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online