Katibu CCM Ilala aungana na wananchini kupima afya maadhimisho ya kilele cha miaka 41 ya CCM

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/02/katibu-ccm-ilala-aungana-na-wananchin.html
KATIBU wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Ilala, Joyce Mkaungala, amefungua mpango wa upimaji wa afya katika kusherekea kumalizika kwa kilele cha miaka 41 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) , tangua kizaliwa kwake kwenye Uwanja wa Pugu Kajiungeni , Wilaya ya Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

KATIBU wa Chama cha Mapinduzi CCM, Wilaya ya Ilala, Joyce Mkaungala,akipima urefu katika kilele hicho.
Miongoni mwa magonjwa yaliyopimwa ni pamoja na kisukari, tezi dume, ukimwi pamoja na uchangiaji wa damu salama.

Mmoja kati ya wanachama wa CCM akijitolea Damu ,leo katika kilele cha miaka 41 ya CCM.PICHA NA MO7 NEWS
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Joyce, amesema lengo ni kuonyesha ni kwa jinsi gani Chama cha Mapinduzi (CCM) kinavyowajali wananchi katika afya zao ili kuendelea kuwa na imani na chama chao kinachoonesha dhamira ya dhati ya kumnufaisha mlala hoi na masikini.

Joyce, amesema, CCM ni chama kinachojali maslahi mapana ya Taifa, hivyo kitendo cha kuwakutanisha wauguzi kutoka sehemu mbali mbali ni moja ya maadhimio ya kukifanya chama kuwa na dhamira ya dhati ya kusaidia wanyonge na masikini kama Rais John Magufuli alivyosema kwenye ahadi zake kipindi cha kampeni mwaka 2015.

Pakiti ikwa tayari na Damu.
“Hii ni siku nyingine, tumemaliza kusherekea miaka 41 ya CCM, hatuna budi tukawafikia watu waliopo pembezoni tukawasaidia katika huduma za afya, kuna wengine hali zetu zinatofautiana kiuchumi na kushindwa kumudu gharama za matibau na vipimo , kama Chama imara chama cha wanyonge na masikini tumekubali kuwa na wananchi wetu karibu ili kumuunga mkono Rais wetu ,John Magufuli ,kwa jitihada zake za kuimarisha afya za wananchi wake”, amesema Joyce

Aidha, aliwashukuru sana, wauguzi kutoka sehemu mbali mbali kwa kukubaliana na Uongozi uliopo madarakani kutoa huduma hizo bure bila ya malipo na kuwataka waendelee na moyo huo wa kujitolea kwani wanawafanyia huduma hizo ni watanzania wanyonge na masikini na ni faida kwa taifa kuwa na nguvu kazi zenye tija.

Daktari akifunga vizuri pakiti ya Damu.
Pia aliwapongeza sana, Viongozi wa Chama , Katibu wa itikadi na uenezi CCM Taifa , Mh: Pole Pole , kwa kujitoa na kuacha kazi zake kuwafikia wananchi waliojitokeza kupima afya, mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Ubaya Chuma, Katibu mwenezi wa Wilaya , pamoja na viongozi wote wa chama waliojitokeza.

Hata hivyo, alienda mbali zaidi akimsifia Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akidai ni mwanamke mwenye harakati za kweli katika kubadilisha taswira nzima na mfumo wa maisha ya binadamu ya kuleta maendeleo ya kweli.

Amesema kuwa, DC Mjema, ni miongoni mwa viongozi wa kuigwa anafanya mambo makubwa sana ndani ya wilaya yake, amekuwa karibu sana na wananchi katika Nyanja zote na kusaidia kusukuma gurudumu la maendeleo Wilaya ya Ilala.

Msaidizi wa Masuala ya kisiasa na itikadi akimwakilisha,Mkuu wa Wialaya ya Ilala, Sophia Mjema, Odacks John,akizungumza na waandishi wa Habari.PICHA NA MO7 NEWS.
Pia amempongeza Rais John Magufuli, kwa kazi kubwa anazozifanya za kuhakikisha Tanzania ya Viwanda inaendana na ubora wa afya za nguvu kazi kwa kujali huduma za afya kwani sasa mambo yamebadilika na huduma zinaridhisha.
Naye msaidizi wa Masuala ya kisiasa na itikadi akimwakilisha,Mkuu wa Wialaya ya Ilala, Sophia Mjema, Odacks John, amempongeza katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Yoyce, kwa ubunifu wake na kumtaka azidishe maarifa zaidi kwani kitendo cha kusaidia upimaji afya sio kwa Wanachama wa CCM bali hata kwa Vyama vingine.

Mwananchi akijitolea Damu,PICHA NA MO7 NEWS
Pia, amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akimtaka azidishe kasi ya kiutendaji kwani yeye amekuwa chachu ya maendeleo ya Wilaya tangia ateuliwe kushika nyadhifa hiyo.
Katika hatua nyingine, mkazi anayeishi Kigogo Freshi kata ya Pugu , Mwajuma Hassan, amekishukuru Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuwajali wananchi na kumtakia maisha marefu , Rais John Magufuli ,katika kupamabana na mafisadi ili kila mwananchi afaidi keki ya Taifa.

Wananchi wa Pugu wakiwa wamejitokeza kwa wingi katika zoezi la kupima afya na uchangiaji wa Damu salama,PICHA NA MO7 NEWS.
Dr Manage Frank, Mkurugenzi wa CCPmedicene, amesema ni lazima kila mwananchi ajenge utaratibu wa kupima afya, kwani kutamsaidia kuokoa maisha na vifoo visivyo vya kilazima , kwani baada ya mtu kugundulika na ugonjwa atachukua tahadhari na kuanza matibabu mapema.
Aidha, Mratibu wa huduma za maabara Manispaa ya Ilala, Petrobas Hassan, amewataka wananchi kuwa na utaratibu wa kuchangia damu, kwani hali za kuchumi zinatofautiana, pia Hospitali nyingi zina uhaba wa damu, hivyo kujitolea kutaokoa maisha ya wengine ,na kuwaomba wakazi wajitokeze kwa wingi kuokoa afya za wengine baada ya watu kupatwa na ajali na upungufu wa damu.