RC Makonda aridhishwa na kasi ya ukarabati Mabasi ya Jeshi

  
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salam, Paul Makonda, leo ametembele mradi wa ukarabati wa Mabasi  yanayoendelea kufanyiwa marekebisho kwenye karakana ya Magari Mwandege, Wilaya ya Mkuranga, Mkoa wa  Pwani na kuridhishwa na kasi na jitihada zao.


 Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkoani Pwani Wilaya ya Mkuranga, RC Makonda amempongeza wa Dar Coach , Manmeet La, kwa jitihada za dhati katika kasi ya ukarabati wa mabasi hayo jambo ambalo litasaidia kuimarisha ulinzi mkoa wa Dar es Salaam.
RC Makonda, amesema maendelo ya wananchi huletwa na amani na usalama kama mahala patakuwa haukuna usalama ni vgumu kufikia malengo .
Amesema kuwa , katika mabasi hayo yanayotarajwa kumalizika siku za hivi karibuni yatakuwa na sehemu mbali mbali za kuchajia simu, ambapo katika upande wa pembeni mwa basi na kwenye kochi zitawekwa sehemu za kuchajia ili kuhakikisha Askari wote wanapatikana muda wote kwa nyakati tofauti kutoa huduma kwa jamii.
Miongoni mwa lengo kuu la ukarabati huo wa mabasi yapatayo 11, ni pamoja na kuhakikisha vyombo vyote vya ulinzi hapa nchini ikiwamo Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi, pamoja na Jeshi la Magereza wanakuwa na ulinzi mzuri .
Pamoja na ukarabati wa mabasi hayo, RC Makonda amehakikisha kuboresha gari la Matarumbeta  la Jeshi la Polisi kulifanyia ukarabati ili lionekane kwenye muonekano mzuri.
RC Makonda, amewataka wale wote wenye kuhitaji huduma za ukarabati wa Mabasi yao wasisite kwenda Dar Coach na watajionea utofauti na hatimaye mabasi yao yatakuwa na taswira mpya.
"Napenda kuwahakikshia ukarabati unaendelea vizuri, tunafanya hivi kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika mkoa wetu, tunataka wananchi wawe salama pamoja na mali zao, tunategemea mwsihoni mwa mwezi huu tutapata mabasi 5 na mengine 6 yaliyobakia kasi itaongezeka na kuyapata yote 11 naomba na wengine wajitokeze kusaidia huduma nyingine ili  maendeleo yazidi kukua kwa kasi ".Amesema RC Makonda
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Dar Coach, Manmeet Lal, amesema ukarabai unaendelea vizuri, mpaka sasa kuna jumla ya mabasi 11, huku mabasi 5 yakiwa ni ukarabati na 6 ni kwa ajili ya matengenezo mapya.
Pia Mkurugenzi huyo amesema jumla ya shilingi milioni 830 za kitanazania zitatumika kufanya matengenezo hayo ambapo milioni 630 yatatumika katika matengenezo ya mabasi 6 na milioni 200 zitatumika ukarabati wa mabasi 5
Naye Kaimu Kamishina wa Jeshi la Magereza (DCP), Augastine Mboje, amesema ameridhishwa na utendaji wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda kwa kazi nzuri anayofanya ya kuimarisha ulinzi na usalama kwa vyombo vyote hapa nchini na kumtaka aendelee na moyo wa kujitolea  ili hali ya amani na usalama iwe na uhakika kwa wananchi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online


Related

habari 3646501206438002958

Post a Comment

emo-but-icon

item