RC Makonda akata mzizi wa fitina Tanzania ya Viwanda

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda, ameanza kazi ya utekelezaji wa Ujenzi wa Viwanda baada ya  kutembelewa na Wachina Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam..

Hatua hiyo imekuja baada Waziri wa TAMISEMI, Selemani  Jafo, kutoa agizo la kila Mkoa kuwa na Viwanda vipya 100 na kutekereza ipasavyo sera ya Serikali ya Viwanda.


Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dares salaam Leo, RC Makonda, amesema lengo la kukutana na Wachina hao ni kuhusu uwekezaji mkubwa utakaopelekeea Mkoa wa Dar es Salaam kustawi kwa kasi katika nyanja ya viwanda na kunufaisha wananchi wake pamoja na Serikali kwa ujumla.


Hata hivyo, mesema kuwa ili kufanikisha dhana ya uchumi wa Viwanda, Serikali haina budi kuwapa msukumo na ushirikiano wa karibu Wanasayansi utakaowezesha kuibua Viwanda vingi zaidi pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa maligafi za kilimo nchini.


RC Makonda, amesema hatua za awali zimefanyika na mazungumzo hayo yalianzia nchini China alipokuwa ziarani hivi karibuni na kukutana na wawekezaji mbali mbali pamoja na wafanya biashara wakubwa.


'Huu ni mwanzo, Wageni hawa hawakuja kubahatisha wapo katika kusimamia maendeleo, watakapo wekeza faida itakuwa kwa Taifa letu na wananchi wetu, jukumu lililopo mbele yetu ni kuwatafutia eneo kubwa la uwekezaji, pia nawaomba wale wengine watakao kuja Ofisini kwangu nawakaribisha kama watahitaji kuwekeza nje ya Dar, tutawaunganisha na Wakuu wa Mikoa husika". Amesema RC Makonda 

Pia amefafanua kwamba, kutokana na uhusiano mzuri wa nchi ya Tanzania na China, anaimani  wawekezaji hao watakubaliana na hali ya uwekezaji hapa nchini hususani mkoa wa Dar es Salaam kwa kufanya Jijini la Dar kuwa la utafutaji na biashara.

KONDA amesema hayo Mara Baada  ya kuhakikishiwa na wachina hao juu ya kutanua wigo wa kibiashara Kati ya serikali ya Tanzania na ya UChina. 

Amesema kkuwa hatua iliyoko ni kutafuta eneo la uwekezaji (Industrial erea) ambapo jumla ya Kilometa za mraba Milioni 5 zitahitajika.


Aidha Rc Makonda, amesema baada ya uwekezaji huo , Vijana wa Kitanzania watanufaika kwa kupata ajira huku akiwaomba wale wote watakaobahatika kuajiriwa watumie fursa hizo kikamilifu kwani wapo tayari kuwapa ushirikiano wa kutosha.

Amesema uwekezaji wao utakuwa na Faida kwa nchi zote mbili kikubwa wanachohitaji ni ushirikiano kutoka serikali ya TANZANIA. 

"Tuna imani na RC Makonda, hata juhudi za Rais Magufuli tumeziona na kuzichukua kama njia moja wapo ya kudumisha urafiki kwenye sekta nzima ya biashara na uwekezaji, tunataka kupanua wigo katia ya Tanzania na China naimani kwa Tanzania tutafanikiwa  kutokana na uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi zetu hizi mbili".Amesema Xiezengyi

Moja ya mkakati wao kwa sasa ni kuwekeza katika Mkoa wa Tanga mabapo uwekezaji huo utaunganisha moja kwa moja na Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kiwanda chao watakachokijenga Kunduchi na kuwanufaisha wakazi wa Dar ,huku uwekezaji huo ukitarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani  bilioni 3.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania,  bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online


Related

habari 1271740777525159194

Post a Comment

emo-but-icon

item