DC Hapi ataka chemba korofi, mitambo majitaka kufanyiwa kazi

https://raiatanzania.blogspot.com/2018/01/dc-hapi-ataka-chemba-korofi-mitambo.html
MKUU wa Wilaya ya Ilala, Ally Hapi, amewataka wale wenye
majukumu ya kusimamia chemba korofi zote zilizopo Wilaya ya Kinondoni pamoja na
Mitambo majitaka wafanye kazi kwa bidii
na kuwa wepesi kutembelea maeneo sugu ili kubaini maendeleo na kasi ya kazi
iliyopo.
DC Hapi aliyasema hayo hivi karibuni mara baada ya kutembelea maeneo yaliyo na
shida ya Chemba korofi ambapo aliwataka Dawasa na Dawasco kuhakikisha kazi hiyo
inakamlika kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha afya za Wananchi na kulinda
miundombinu ya bara bara katika kuzuia upotevu wa pesa inayotumika kukarabati
bara bara.
Akizunguma na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, DC
Hapi alisema hafurahishwi na kasi ya maji taka iliyopo kwenye wilaya yake huku
akiwataka wataalamu wanaosimamia miradi hiyo kuwa wabunifu wa kutatua matatizo
kwa haraka na kuwa na majibu sahihi.
Aliwapongeza Dawasco na Dawasa kwa kazi nzuri walioifanya ya
katika eneo la maji safi lakini hakuridhishwa na kasi ya kupambana na kuzuia
maji taka yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira hivyo kuwaomba
waongeze a kasi kwenye upande wa
kudhibiti maji taka ikiwema kumaliza
tatizo la chemba zote sugu.
Pia aliwapongeza Dawasa na Dawasco kwa jitihada walizozichukua
za kuwa na eneo kubwa la Treatment Pond eneo la Kilonga Wima lililopo Jangwani
Beach utakao gharimu kiasi cha dola za Kimarekani milioni 65 kwa ushirikiano
kati ya Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia , ambapo watajenga mtambo wa
kusafisha majitaka utakao kuwa na uwezo wa kusafisha mita za ujazo 16,000 kwa
siku na utajumuisha mfumo wenye urefu wa Kilometa 97 utakaopita eneo la Mbezi
Beach, Kawe, Tegeta na maeneo mengine jirani.
Aidha alitoa muda wa mwezi mmoja Chemba korofi iliyopo eneo
la Mwenge iwe imekamilika na kila mradi
uwe umemalizka ili kuokoa pesa za Serikali kupitia kodi za Wananchi.
Kwa upande wao, Kaimu Mkurugenzi Maji taka DAWASCO , Shabani
Mkwanywe, alisema moja ya changamoto zilizopelekea DAWASCA ni uchakavu wa
mifumo ya maji taka pamoja na mabomba mengi kuwa chakavu kutokana na kuwa na
umri mkubwa huku akisema mengi yalitengenezwa kipindi cha miaka 1950-1970 huku
wakazi wa Dar es Salaam wakikadiriwa kuwa laki tano tofauti na sasa kufikia
takribani milioni tano.
Mkwanywe alisema mabadiliko ya upanuzi wa Jiji na maendeleo
yake yamechangia kwa kiasi kikubwa kuwepo na chemba mbovu kwani Jiji
limeendelea kila uchwao mijengo inazidi kuongezeka na huduma ya Chemba inazidi
kuongezeka kwa kasi hivyo wapo katika kuhakikisha wanafunga Pump mpya ili kutatua
tatizo.
Naye Kaimu mkurugenzi wa huduma za ufundi DAWASA,
Modesta Mushi, alisema lengo la mradi wa Mtambo wa uchakataji Maji wa Kilonga
wima ni kuongeza uwezo wa mfumo wa ukusanyaji wa Majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Alisema jumla ya kilometa 563 za mabomba ya ukubwa
mbali mbali ya ukusanyaji majitaka , yatakusanya majitaka na kuyamwaga katika
mitambo mikubwa mitatu itakayojengwa Mbezi, Jangwani na Kurasini.
Mushi alisema mitambo hiyo mipya itazalisha gesi
asilia na umeme kwa ajili ya kujiendesha, hivyo kupunguza matumizi na gharama
za umeme.
maji yatakayokuwa yamesafishwa yatauzwa na kutumika
katika shughuli mbali mbali kama vile kupozea mitambo na umwagiliaji huku tope
litakalo bakia baada ya mchakato huo litatumika kama mbolea kwa ajili ya kilimo
pamoja na bustani za majani na miti ya kivuli na hivyo kupendezesha Jiji la Dar
es Salaam.
“Mtambo huu utakuwa unauwezo wa kusafisha mita za
ujazo 200000 kwa siku, mfumo wa mabomba yenye urefu wa kilometa 370
yatakayolazwa kuanzia Ubungo hadi Jangwani, Kinondoni, Mwananyamala, Msasani,
kati kati ya Jiji na Ilala”Alisema Mushi
Awamu ya kwanza ujenzi wa mtambo utasafisha mita za
ujazo 25,000 za majitaka kila siku na mabomba ya kilometa 17.43 yatakayojengwa
katika mitaa ya Magomeni, pia katika awamu ya kwanza bomba linalomwaga majitaka
baharini litaacha kutumika na badala yake yatakwenda kusafishwa katika mtambo
huo ambapo jumla ya dola za Marekani milioni 90 zitatumika.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.raiatanzania.blogspot.com ku-install App ya raiatanzania, bila ya kuingia websiteTweet@Raia Tanzania online, youtube@Raia Tanzania online TV, Fb@Raia Tanzania online, insta@raia Tanzania online