Wagonjwa waliogundulika na hali mbaya kutibiwa China:RC Makonda





 Rc Makonda akisalimiana na baadhi ya wagonjwa walifuka na kupatiwa huduma ya matibabu katika Meli ya China katika bandari ya  jijini Dar es Salaam
Hawa ni Baadhi ya wagonjwa ambao tayari wamekwishapatiwa huduma 

 Zoezi la Upimaji wa Afya na Matibabu Bure Ndani ya Meli ya Jeshi la Jamuhuri ya Watu wa China Leo limeingia Siku ya Pili ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. PAUL MAKONDA amesema Wagonjwa ambao wataonekana kuwa na Hali mbaya watasafirishwa kutibiwa Bure Nchini China.

 MAKONDA amesema Ofisi yake itaratibu utaratibu wa Hati za Kusafiria (Passport) ili kuhakikisha Wagonjwa wanapatiwa Matibabu ili kuokoa Maisha yao.

Aidha amesema Wagonjwa Wanaopangiwa kulazwa kwenye Meli hiyo yenye Vitanda vya Wagonjwa zaidi ya 300 wanapatiwa huduma za Malazi Bure ikiwemo Chakula, Vinywaji, Mavazi.

Aidha MAKONDA amekemea tabia ya baadhi ya Watu wanaochukuwa Kadi za Matibabu kisha kuziuza kwa Watu.

MAKONDA amesema kasi ya utoaji wa huduma  ni nzuri hivyo anaamini hadi siku ya Mwisho ya Zoezi la Upimaji Wananchi wote waliopatiwa namba watakuwa wamehudumiwa.

Katika kuongeza nguvu kasi ya Upimaji Madaktari kutoka JWTZ,  Muhimbili na Hospital za mkoa wa Dar es salaam Ikiwemo Amana,  Temeke na Mwananyamala wanashirikiana na Madaktari wa China katika kutoa huduma.

Related

habari 4302228220958223546

Post a Comment

emo-but-icon

item